LHRC mna wajibu wa kukanusha upotoshaji na madai ya USA

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,119
7,701
Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na Haki za binaadamu LHRC ina wajibu wa kutoa tamko la kukanusha juu ya upotoshwaji uliotolewa na Marekani juu ya kinachodaiwa kuwa nchi yetu inavunja haki za binadamu.

Nasema hivyo kwakuwa taasisi hiyo ipo nchini kwa kazi kubwa ya kusimamia na kulinda haki za binadamu na pia kuibua aina yoyote ya ukwiukwaji wa haki za binadamu.

Ripoti ya kila mwaka inayotolewa na taasisi hiyo haionyeshi kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

Kilichofanywa na Marekani ni upotoshaji wa maksudi wenye nia ya kuchafua heshima ya nchi yetu.

Kitendo hicho kilaaniwe kwa nguvu zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yote chanzo mbinyo wa democrasia uliokuwepo ndani ya CM uliosababishwa na Ndg. JMK.
 
sasa kama wanatishiwa maisha na Yona..huo ujasiri wakutoa hizo taarifa watautoa wapi ?
 
Siyo kila kinachoamuliwa na watendaji wa Serikali ya Marekani kinakubalika na raia wake... Hebu angalia hii>

 
Hio taasisi hadi muda huu imeshatoa tamko lolote la maafa ya moshi?

BTW nafikiri toka Mama Kijo Bisimba apate ile ajali baada ya uchaguzi, hawa jamaa ilikuwa kama wamezibwa mdomo.

Mimi nimekuja kuwasikia mwaka jana Tito alivyokamatwa na polisi.
 
Back
Top Bottom