chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,819
- 26,180
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.
Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Bi Imelda Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi na rasimi za michakato ya maridhiano toka kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya wananchi juu ya viongozi wao, tume na mchakato mzima wa chaguzi za kidemokrasia Zanzibar.
Wakati huo huo, chama cha kijamii CCK kimemsimamisha kazi na uanachama naibu katibu mkuu wake wa Zanzibar Ali Khatib Ali ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa na ZEC Oktoba 2015.
Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda amesema chama kimefikia maamuzi hayo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi wake binafsi wa kutangazia umma kuwa CCK itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kinyume na taratibu za chama.
Chanzo: EATV