Level ya elimu kwa wabunge wetu

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
735
Baada ya kupitia c.v za wabunge wetu nimegundua kuwa wapo wengi ambao elimu zao ni ndogo kabisa yaan std 7 na wengine ni za kawaida yaan form 4, form 6, elimu za ufundi, certificate, diploma. Na wachache elimu ya juu kwa maana ya degree hadi phd na professor.

Sasa hebu tuje kwenye utendaji kwa sehemu kubwa bungeni majina yanayosikika ni wabunge maarufu na tunawaona ni hawa wenye elimu ya kawaida kwa maana wasio na elimu kubwa sana ingawa wenye elimu kubwa maarufu wapo japokuwa sio wengi ukilinganisha na hawa wenye elimu ya kawaida.

Na ili mbunge uwe maarufu lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kuuliza maswali yenye maslahi moja kwa moja kwa wananchi na Serikali.
Sasa ni kwanini hawa wabunge wenye elimu ya kawaida wameonekana kuwa na majina zaidi ya wale ma phd holders ambao tulitegemea ndio wao waanze kuonekana na kuwa na majina makubwa kutokana na elimu zao na kwa kuwa na ujuzi na utaalam wa mambo mengi ukiwalinganisha na hawa wenye elimu za kawaida?

Sijajua bado tatizo ni nini kinachopelekea wasomi wetu kupooza wanapokuwa mjengoni ambako tulitegemea kuwaona waki itetemesha Serikali kwa hoja zao zenye mashiko na hatimae kujizolea umaarufu kwa wananchi halafu wale wabunge wengi wenye elimu ya kawaida ndio wafuate nyuma yao.

Wasomi wetu wanashindwa kujipambanua hadi imefika mahali watu wana anza kusema pale mjengoni ni kwa wanaojua kusoma na kuandika kwa maana hata wasomi waliopo pale bado hawaonekani kwa hoja zao badala yake tunaona zikitoka kauli nyepesi ambazo kila mtu anaweza kuzipinga tena kwa urahis hata kama hana elimu kubwa na akaonekana yuko sahihi kwa hoja.

Sasa je, kinacho mfanya mbunge awe machachali mjengoni ni elimu yake au kipaji na ujanja ujanja tu na sio elimu yake? Na kama ni elimu, kwanini wenye elimu kubwa tumekuwa tukiwaona wachache na wao pia kwa sehem kubwa hoja zao ni nyepesi?

Kutokana na hayo nashindwa kuhitimisha na nnapata ukakasi kusema level elimu ya elimu kwa wabunge iweje ingawa ni muhimu sana kwao kuwa na elimu kubwa kwan maamuz yao yana athiri jamii kubwa tena moja kwa moja. Naomba kujua level ya elimu kwa wabunge iweje ili iwe na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
======================

Kalenga kidamali

NawAsiliaha
 
siasa siyo elim ndugu yangu, sasa mbona katika marais woote wa bongo mwenye PHD ndio mbovu kiliko wote, jibu ni kuwa siasa ni field inayo hitaji mambo mengi zaid tu ya elim, japo elim ni muhimu lakin mtu ana Phd ya Plumbing, haiingilian kabsa na siasa.
siasa inahitaji ujanja, dedication, na uzoefu, kwa bongo na uchawi(according to mh Msukuma).
 
Mwanasiasa Elimu sio lazima. Anatakiwa kuwa na general knowledge kama msingi wa kujengea hoja ya kila kitu.
Awe na basics za Geopolitics,Geography, Sheria,HEsabu kidogo,Biashara,Uchumi,Lugha,Mahusiano, Maarifa ya jamii na Sayansi. Hii yote ataipata Sio kupitia Darasani bali Habari za kimataifa CNN,BBC,RT,CCTV etc, Aangalie Documentaries za mambo karibu ya nyanja zote za maisha ya mwanadamu,Ahudhulie Seminars na Workshops nyingi kwa kadili awezavyo, Afanye study tours ndani na nje ya Nchi, Ajifunze Public speaking and persuasions skills, Asome makala na journals mbalimbali zinazozungumzia karibu kila aspect ya maisha ya mwanadamu. Na kikubwa ajue historia ya nchi yake,Nchi jirani na Dunia kwa ujumla, Ajenge mazoea ya kuwa karibu na wataalamu mbalimbali kwa ajili ya knowledge transfer nk.

Kikubwa kabisa ajenge utamaduni kwa kusoma sana vitabu mbalimbali...

Haya yote akiyafanya sehemu ya maisha yake. Darasa la nne au kujua kusoma na kuandika ni Qualification Tosha kabisa kwa mwanasiasa yoyote.
 
Katika siasa kuna wanasiasa wa aina tatu
1. Strategists= Anatakiwa awe amesoma, sio mzungumzaji sana lakini ni mzuri wa kuandaa mikakati ya kisiasa.
2. Whistle blowers: Hawa ndio mafundi wa kuongea wao kazi yao ni kuwasilisha kile walichopewa, hawa hawahitajiki kuwa wamesoma sana, wanatakiwa kuwa wajanjawajanja.
3. Wapiga debe: Hawa ni wale wenye ushawishi kwa jamii ya mahali wanapoishi. Hawa hawajihusishi na siasa moja kwa noja lakini ni wadau muhimu nyakati za kampeni.

N:B, Siasa ni kipaji pia, kuwa mtaalam kwenye physics haitakuguarantee kuwa mtaalam kwenye siasa.
 
Uganda ili kuwa Mbunge wameweka Elimu ya chini iwe kiwango cha A-Level ( Kidato cha sita )

Wabunge wa Bunge la Uganda elimu zao ni 10 wana PhD,147 wana Mastes,200 wana Bachelor,28 wana Diploma 13 wana vyeti.

Wabunge wa Bunge la Canada kwenye PhD 14 kwenye Masters 97 na kwenye Bachelor ni 227
 
Back
Top Bottom