Let us protect academic freedom

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
Niliwahi kuandika kuhusu Academic freedom yafuatayo:-

Academic Freedom ni uhuru wa wanataaluma kuruhusiwa kufanya tafiti na kutoa matokeo ya tafiti zao bila kuingiliwa na mtu yoyote.

Academic freedom haishii tu kufanya tafiti bali kwa mtaalamu yoyote anaruhusiwa kutoa mawazo yake either kwa ku challenge chochote anachohisi kitaleta matokeo chanya kwa jamii.

Si kanisa, wala Serikali, au mfadhili mwenye mamlaka ya kuzuia taaluma isiwafikie jamii. Serikali au chombo chochote kwa kifupi hairuhusiwi kuzuia au kucontrol knowledge.

Academic freedom huruhusu majadiliano (Debates) kwa lengo la kuupata ukweli. Ni jukumu la kila mwanataaluma kuhakikisha analinda na kuipigania academic freedom.

Kuna mtu akiitwa Galileo alitoa nadharia yake ya copernican ambayo ilielezea kuwa kanisa katoliki lilikuwa likipotosha kuwa jua huzunguka dunia... badala ya dunia kulizunguka jua.

Kwa kusema ukweli huo tena kwa tafiti Galileo aliishia kufungwa na kuteswa mateso makuu na kanisa hadi kufa. Mateso ya Galileo yalikuwa makali hadi kifo kikamkabili.

Mwanalsafa Aristotle yeye kwa kufundisha ukweli tu kwamba Demokrasia inachelewesha maendeleo alipewa Sumu akafa.

Prof Mhongo kwa kusema tu kuwa wazawa hawana fedha za kuwekeza kwenye Gesi na mafuta tuliona yaliyomwandama. Nafikiri huyu hata ukiwamsha usingizini leo atakujibu jibu hilo hilo kuwa hawana uwezo.

Hii ni mifano michache tu ambayo inaonyesha jinsi Taaluma zinavyokinzana na Mamlaka madhara yake hasa kwa wanataaluma wenyewe.

Hakuna dhambi kubwa kama wewe ni mwanataaluma kupingana na taaluma yako inachokuelekeza. Mfano Galileo si mateso ya kanisa yalimuua bali ni msononeko wa Moyo ndio uliomuua kwa kulazimishwa kuikataa nadharia yake ya copernican.

Jamii, watawala, na taasisi nyinginezo zinapaswa tuheshimu pia academic freedom kwa manufaa ya nchi na kuupata Ukweli. Ukizuia wanataaluma kuongea ni umezuia maendeleo yako mwenyewe.

#Tatizo tulilonalo kwa sasa hapa kwetu wanataaluma nao hawaaminiki sana wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi. Wengi wa wanataaluma wamegeuka kuwa wanasiasa, Hivyo wanapotaka kutoa mawazo yao yanachukuliwa kama siasa.

#Wakati tukiendelea kushangaa na kumpongeza Dr Mwele Malecela basi tufikiri pia umuhimu wa kulinda na kutunza Academic Freedom.

 
Njoo Tz na maujinga yako ukumbane na law
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…