Leonardo da Vinci Tanzania

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,234
Reaction score
1,503


Kama picha hii ingekuwa ni ya kuchorwa. Basi ni lazima ingekuwa imechorwa na si mwingine, ni gwiji Leonardo di ser Piero da Vinci. Picha hiyo imejaa maelezo yote kuhusu hatima ya sakata la makinikia ya shaba kati ya serekali ya Tanzania na kampuni ya Acacia. Picha hiyo ina maelezo yote muhimu kuhusu maafikiano kati ya Tanzania na Acacia. Hata wewe jaribu kutumia muda kuangalia picha hiyo, na unaweza pata taarifa zote. Hiyo itakusaidia siku taarifa hizo zikitangazwa, wewe utakuwa unaendelea na shughuli zako bila kuathirika kisaikolojia.
 
Tafadhali wakuu. Mwenye photoshop karibu anisaidie ku-blurry background ya hiyo picha. Hakika taarifa zitazidi kuwa wazi na tutaona vitu tofauti kabisa.
 
Sioni hata dalili za kulipwa angalau trillion 5 tu!
Kweli tupo nchi za ulimwengu wa tatu yaani kutoka trillion 108 mpaka kutopata chochote!!
 
Huyo mzungu hako ka mdomi alivokakunja ni ishara ya dharau kubwa.. Huku Magufuli akionekana yupo serious na mwingi wa hasira..

Maana ya picha: Mzungu kaonesha dharau ,, Magu kaonesha hasira na msisitizo

Hitimisho: Jamaa hawapo tayar kulipa ndururu yoyote
 
Ila huyu Mzungu ana madharau sana...check anavyomtizama Mkulu.
 
Hakuna kulipwa hapo zaidi ya changa la macho

Ukizingatia na yale aliyoyasema Prof. Kabudi ndio kabisaaa.
 
Hawa jamaa wako smart far away from us. Natamani hiyo imani initoke sikumoja. Lakini kila kukicha, viongozi wetu wananithibitishia imani yangu iko sawa. Nachukia.
 
Wewe endelea kuchochea wale wazee wa Noah wakuone
 
Mnakosea Sana Yaani Hii Ni Dhahiri Kuwa Mleta Mada Unachochea Jambo
Watch It
 
Mimi naamini ipo uwezekano wa mtu mmoja kuwa sahihi against wengi na pia upo uwezekano wa kundi kubwa kuwa sahihi against mtu mmoja.

Na hiki ndicho kinachotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…