Eddy Love
JF-Expert Member
- Jul 25, 2011
- 13,654
- 8,553
Kwanza unatakiwa kujua hakuna mapenzi ambayo ni matamu kama mapenzi ambayo yana maendeleo na yenye maisha mazuri. Hata siku mkiwa mko kwenye show zenu huku mna uhakika wa maisha huwaga zile show zinakuwa amazing sana mana zinakuwa hazina stress.
Sasa leo kuna vijana wengi wanakomaa kwenye mahusiano ambayo kwanza hayana furaha japo wanalazimishia furaha. Kwanza kijana unatakiwa kupiga mahesabu kuwa toka umeanza mahusiano na mpenzi wako maisha yanaenda mbele au yanarudi nyuma.
Ukiona maisha yanarudi nyuma basi jinasue kwenye hayo mahusiano. Kwanza siku hizi vijana wanakomaa kuingia kwenye mahusiano na mabinti wadogo na wazuri kwa ajili ya kufurahisha matamanio yao ya sex tu.
Sasa shida ya vibinti hivyo unakuta havijui chochote kuhusu maisha yani hajui kuna kupata au kukosa siku akipiga kizinga huna ananuna. Uko kwenye mahusiano na binti ambaye anajua majina yote ya club mpaka club zingine anaingia bure kwa sababu ashazoeleka wewe bado unakomaa naye.
Tena vijana wengine unakuta anajinyima kabisa yeye anampa mwanamke yani anapigwa kizinga anatoa huku anatukana moyoni eti kinachofanya ajitoe muhanga anaogopa
akimnyima wengine watampa.
Sikia nikuambie kitu, hawa mabinti wa siku hizi ambao hawayajui maisha jinyime weeh siku umeishiwa kabisa usifikiri atabadilika ndio kwanza atakuacha. Sasa wengine unakuta wanakutana na mwanamke ambaye amemzidi umri anampenda lakini anaona noma masela watamcheka.
Acha nikuambie hata mwanaume kuna muda anahitaji kuwa na mwanamke wa kumuongoza ukikuta umepata mwanamke amekuzidi umri ila anayajua maisha usiogope maneno ya watu kuwa naye ukiwa hasa unajua malengo yako na kile ambacho unapata.
Tambua kabisa kuwa na mahusiano na binti ambaye hajawahi kuwaza maisha zaidi ya starehe ni kutengeneza cancer ambayo itakuja kukumaliza mbeleni.
SASA ENDELEA KUJITOA MUHANGA KUVIRIDHISHA HIVYO VIBINTI UNAFIKIRI UKIISHIWA ATAKUONEA HURUMA WAKATI NDIO KWANZA ATAENDA KUCHUKUA KIBABU KAMA BABA YAKO ILI AENDELEE KULA STAREHE.