Leo katika Historia: GENOCIDE (mauaji ya halaiki) 09 duniani ambayo hukuwahi kuyasikia

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Ukisikia mauaji ya Halaiki(genocide) akili inakimbilia RWANDA, SOWETO na HOLOCUST(waisrael walivyouliwa na WANAZI). Leo nakupa Mauaji yaliyosahaulika lkn nayo sio mchezo.

01: WAJERUMANI WALIVYOSAFISHA KABILA LA WAHERERO
800px-Surviving_Herero-600x400.jpg

Gefangene-Hereros-in-Deut-007.jpg


Baada ya kusikia fununu ya MAdini NAMIBIA, Wajerumani walikuja na kutawala pwani ya nchi hiyo na kukaa katikati ya kabila la waherero. Kosa kubwa wenyeji walipojifanya wabishi. Walizungukwa pande zote, Upande uliobaki ulikuwa ni JAngwa ambalo visima vyote vya maji mjerumani alivitia sumu. Ukimbie unywe maji ya sumu au ufe na kiu jangwani au ukutane na risasi. Asilimia 80 ya wenyeji wote waliuwawa kikatili sana bila huruma.

2:WASOVIETI/USSR WALIPOHAMISHA JAMII NZIMA ya WACHECHNYA
crowd_detail-e1380312707251.jpg

0_e4e17_ee3c8a4c_XL.jpg

Kulizuka fununu kuwa WACHECHYA na WAINGUISH walikuwa wanawasaliti warusi wenzao WW2. Kuwapa adhabu serikali iliamuwa kubeba wote kwenye magari na kuwafukizilia maporini bila kumsamehe hata mmoja. Kila aliyebisha alikutana na RISASI. Wachechnya waliuwawa karibu 50% kutokana na sakata hili lililoitwa “Operation Lentil.”.

3:HAITI:MAUWAJI YA PARSLEY/EL CORTE au (KUKATWA)
SfPvSkP4vQ_1399051194010.jpg

Ukabila usikie tu redioni. Hii ilikuwa ni vita ya kikabila. Wadominika walipanga kuwauwa WaHAITI karibu wote nchini mwao chini ya DIKTETA Rafael Leonidas Trujillo. Njia pekee ya kumtofautisha Mdominika na MUHAITI kwa walioleta utata kuwatambua ilikuwa matamshi ya hilo neno/ua PARSLEY, wahaiti walikuwa hawawezi kulitamka vizuri kutokana na Lugha yao. Wote walioshindwa waliuwawa kinyama. Kuepusha risasi zisiishe mapema, Hapa ilikuwa ni Mapanga na marungu asubuhi na mchana.

4:TAIPEI REBELION: CHINA WATU ZAIDI YA 20mil WALIPOTEZA MAISHA.
taiping-rebellion-scroll.jpg

Hapa ilikuwa ni vita kati ya jamaa aliwaaminisha watu kuwa yeye ni MDOGO WAKE YESU. Akitawala karibu 1/3 ya nchi yote Hong Xiuquan. Akiongoza jeshi dhaifu kabisa kwa nia ya kuondoa kamali,uonevu, ndoa za wake wengi etc, China ilijikuta chini aya vita vya miaka 10 na kuacha raia zaidi ya 20MIL wakifa na mamia kupotea.

5:UTURUKI DHIDI YA WANAVIJIJI WAASI
Turkish_soldiers_and_local_people_of_Dersim_region.jpg

baada ya kupiga picha inasadikiwa wote hao waliuwawa na hao wanajeshi
Wanakijiji wa eneo la DERSIM, walipoleta ubishi kuwa chini ya serikali ya UTURUKI badala yake wakang'ang'ania sheria na taratibu zao, Jeshi lilitumwa, Makabila matatu yaliyojisalimisha yaliuliwa wote, Wakina mama na watoto waliokimbilia kwenye Mapango, Yalifunikwa na mawe, moto ukawashwa na wakafa kwa moshi.Inakadiliwa kwa siku moja watu karibu 2MIl waliuliwa na wengine kutekwa.

6: DICTETA Wakirusi STALIN alipoua Mamilioni UKRAIN kwa Njaa.
165217352.jpg

famine-victims-02.jpg

Waukraini walipata upenyo baada ya kuanguka utawala wa CZAR urusi wakataka kujitawala. Jenelali Stalin alipochukua Madaraka akaliona hilo.Pia Vradmil LENIN alikuwa kaishaweka mikakati ya kurudisha maeneo yote. Wao wakambishia na kuendelea na HARAKATI. Kwanza alikamata wasomi waliokuwa wanahojihoji 5000 na kuwaua wote, Akachukua mashamba ya raia yote. Akawapa adhabu ya njaa hadi nchi nzima isalimu amri kwake. Inasadikiwa kwa sababu ya njaa kila siku watu 2500 walikuwa wanakufa, na walifika watu karibu mil5.

7:MAUWAJI YALIYOFANYA NA WAZUNGU DHIDI YA WAMAREKANI ASILIA (wahindi wekundu)

armenia1.gif


Mamilioni ya hawa jamaa waliuliwa bila huruma. Ila hapa tutuzaungumzia kabila dogo tu la MOQUI katika mji ulioitwa AWATOVI huko ALIZONA. Wahispania Makasisi walifika wakawalazimisha jamaa kuwa wakristo wakagoma. Ikabidi liitwe jeshi, maana wakazi waliwachukia wahispania na wachache waliobadili dini. Wanaume wakiwa kwenye sherehe Walivamiwa na kuuliwa. Wanaume wote. Wanawake na watoto wakachukuliwa mateka. Wakiwa njiani wakabishana wawapeleke wapi, wakaamua kuwaua woote ili kujipunguzia mizigo.

8:Jean Jacques Dessalines alipoigeuza HAITI kuwa taifa la watu weusi 100%
800px-Haitian_Revolution-e1380311066636.jpg

massacre2.jpg

Kile alichoshindwa kinjekitile wa MAJIMAJI Haiti iliwezekana. Mzungu alikimbizwa na watumwa nchi ikapatia uhuru chini ya mkono wa watu weusi. Baada ya kiongozi wa mapinduzi kuuwawa aliyemfuatia alipinga idea zake za kuwavumilia wazungu na machotara. Amri ilitolewa Kuuwa WAZUNGU WOTE nchi nzima. Hakuishia hapo tu alipita kila mji kuhakikisha agizo linafuatwa. Katika mji mkuu tu WAZUNGU zaidi ya 800 waliuwawa kama wanyama na wengine kukimbia. Ilikuwa revenge ya aina yake. Hadi kesho haiti ni nchi ya watu weusi tu asilimia karibu mia kwa baara la Barani AMERIKA.

9:VITA VYA BIAFRA - NIGERIA
Ojukwu-military-g-009-e1406632361529.jpg

The-Forgotten-War-1.jpg

biafra.jpg

Tofauti na tanzania tunamakabila mengi yanayopendana, na Nyerere alisaidia kikubwa, Hii haikuwa hivyo Nigeria. Wanamakabila zaidi ya 300 na yalikuwa karibu karibu kilichosababisha ugomvi mara kwa mara.Tatizo lilianza pale Kabila/kundi kubwa la IGBO walipojikatia nchi na kutengeneza nchi yao ya BIAFRA eneo tajiri kwa mafuta. Serikali haraka ikataka kuwarudisha. Kwa mbinu katili kabisa hata kuzuia chakula na maji yasielekee BIAFRA. Inasemekana kila siku walikuwa wanakufa watu zaidi ya 5000 wengi wao IGBO. Watu zaidi ya Milioni 3 walikufa hadi vita kuisha.

HII NDIO DUNIA ILIYOJAA KILA AINA YA MATUKIO.


SEMA CHOCHOTE.
 
Kwa kweli hii history mimi pia nimeipenda sana haya ndio mambo ya maana kukumbushana dunia ilivyokuwa na ilikotoka na inakokwenda. Siyo yale ya masupastaa wa bongo hata kama kanunua chupi kariakoo ya bei poa utasikia mtu kaja hapa jukwaani ooho flani Kawa millionaire kanunua chupi UK kwa dollar 5000 hatuyataki hayo tunataka story kama hizi
 
Umetukumbusha Vyema ili tuipende amani na kupenda maisha japo saa zingine tunakosa mahitaji lakini at least hatujawahi kushuhudia hayo Mungu atuepushe
 
Kazi nzuri mleta uzi, hii dunia ina mambo, kama Unaweza utuwekee na ile ya Zaire alichofanya Mf Leopard.
 
Kuna hawa wanaojiita kuwa ni wakristo kutoka hispania waliwalazimisha native americans wawe wakristo hawa ni Majesuits waliokuwa na uwezo wa kuua kwa orders za General hii ndio ilikuwa taasisi ya kijasusi ndani ya kanisa.This is history in application!
 
Dah, nimekumbuka mbali sana, vita vya wenyewe kwa wenyewe Sierra Leon, mwaka 1996 nakumbuka vita vilianza mida ya tisa mchana tukiwa home, jamaa walizingila makazi ya wafanyakazi Wa UN walirusha sana risasi kabla ya kuja kupewa msaada na jeshi la serikali. Wakati tunaondolewa mnaambiwa kabisa toka na nguo uliyovaa tu. Vita isikie tu, tena isikie mbali tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom