Leo husuta ishi kwa tahadhari

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,557
Reaction score
59,403
HAYA maisha yamesheheni sana umaridhawa. Je, sikukwambia?

Life is so wonderful, didn't I tell you?

Leo inapofika, inaweza kukushangaza kuhusu jana.

Leo hupatanisha maadui wa jana. Hufarakanisha marafiki wa jana. Leo huwafanya waja watamke kuwa ya jana ilikuwa kazi ya Shetani.

Mmh! Leo husuta na kusimanga. Leo hunyenyekeza. Zingatia hata leo itakuwa jana pale kesho itakapoitwa leo. Kuwa makini mwana!

Siku zote ishi kwa tahadhari ya kesho. Tambua kuwa kesho si tatizo la leo, isipokuwa pale hiyo kesho itakapogeuka leo. Halafu ya leo yakatamkwa ni ya jana.

Jana inapogeuka leo, basi leo husuta watu, huwaumbua, huwalazimisha kuomba msamaha na kumsingizia mno Shetani.

ISHI KWA TAHADHARI
 
Umeishia kuzungurukazunguruka tu.

Leo ni leo jana ishapita hiyo. Doa linamaana kubwa katika maisha.

Kaa kwa kutulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…