Utawezaje kuitoa madarakani CCM wakati inawafanyia mambo mazuri wananchi? Acha kutisha watu wewe huwezi hata siku moja ukaleta mambo ya Libya au Misri. Na yakitokea mwanao ndio atakuwa wa kwanza kufa.WE MTOA MADA, NAKUJIBU KAMA IFUATAVYO:- ISIPONG'OKA CCM MAENDELEO ITAKUWA NDOTO KATIKA NCHI HII.
Ccm ni PAKA maendeleo ni PANYA, ILI PANYA AISHI LAZIMA PAKA AONDOLEWE TENA KWA NGUVU KAMA ILE YA MISRI, LIBYA n.k
Mbona sisi tunakula bata tu. au unataka serikali ikuleteee mkate nyumbani kwako? CCM nambari one Afrika nzima. Hata CCM ikigombea Kenya inashinda.Maendeleo hayawezi kuja bila kuiondoa CCM ndiyo maana lengo kubwa la kwanza ni kuiondoa CCM madarakani,maendeleo hayaji bila kuwa kitu kimoja ndiyo maana wameungana ili wawe kitu kimoja,maendeleo hayawezi kuja palipo na tofauti ndiyo maana wapinzani wameweza kumaliza tofauti zao na wameungana vinginevyo wasingeweza kuungana.
Soma hii hapa chini
chanzo: HATARI!! WAFUASI CUF, CHADEMA WAONESHANA UBABE MIKUTANONI... - ziro99blog
Utawezaje kuitoa madarakani CCM wakati inawafanyia mambo mazuri wananchi? Acha kutisha watu wewe huwezi hata siku moja ukaleta mambo ya Libya au Misri. Na yakitokea mwanao ndio atakuwa wa kwanza kufa.
Acha kutumia hisia vitu vinaenda kwa utaratibu.
Wazo la kuiondoa ccm linakuja kwanza maana ni kama unataka kupanda maharage shambani, kusafisha shamba ndio kitu cha kwanza na mavuno ndio maendeleo huku magugu yakifananishwa ccm.
Hivi kama Chenge/EL wanaweza kuungana na Sitta kupitisha katiba ya ccm kuna ubaya gani cdm na cuf kuuanga pia kuikataa!??
Hivi vyama kila kimoja kimeanzishwa kwa maelengo yake na kinafanya mambo yake lakini kwa mara ya kwanza katika historia yao kuna sababu iliyo wazi na vyote vimegongana hapo, nayo ni Katiba Mpya ambayo kwa wenye akili wanajua wazi kuwa ndilo suluhisho la matatizo ya sasa hapa Tanzania. Yakiibuka matatizo mengine huko mbeleni basi watakaokuwepo nao watatengana au kuzidi kuungana kulingana na yatakavyoonekana.
Lengo ni yote mawili..
Unapokata mti japo utakata shina lakini pia inabidi ung'oe na kisiki
Ccm itoke kwanza,hayo mengine mbele ya safari!
Hii akili imewafanya wa Libya hadi leo kutoelewa cha kufanya baada ya kumuondoa Gaddafi. Huwezi kuwa na mpango nusu, lazima mtueleze baada ya kuitoa CCM mtaleta maendeleo gani ili na sisi tujue jinsi ya kuwa hold accountable mkiwa madarakani.
Mbona sisi tunakula bata tu. au unataka serikali ikuleteee mkate nyumbani kwako? CCM nambari one Afrika nzima. Hata CCM ikigombea Kenya inashinda.
Ni kweli CCM inawenyewe na ndio wanaokula bata.Wengine ni wadandiaji wanaosumbuliwa na njaa kali pamoja na ujinga uliosababishwa na CCM.wakenya siyo wajinga wakukichagua chama kama CCM kama CCM wanabisha wakawaulize KANU.