Ulevi huu ndio nisiokubaliana nao......
Mbona wewe ujaachana na mimi? kwa nini unahubiri usichokisimamia? ukiniita Jitu kwangu ni sifa kubwa....tafuta kitabu kinaitwa ALIITWA JITU ndio utanielewa.
Duh! No Fear, umenikumbusha mwaka 1986 nilipokisoma kitabu hicho
Aliitwa Jitu pamoja na kile cha
Wahuni waliobadilika
Nikirudi kwenye mada, ni kweli Godbless anaweza kuonekana alimdanganya Joshua. Vyovyote vile ilivyokuwa, kwamba alidanganya au alifanya makusudi; jambo hilo la kukosa pesa (ambalo lilikuwa ni tumaini la Joshua) lilimfanya aanze kuutumia uwezo ulio ndani yake katika level nyingine. Kama kiongozi alipaswa kupitishwa katika darasa la kutokutegemea mtu bali watu pamoja na uwezo alionao ndani yake.
Ni kweli kuwa unapopitishwa katika darasa kama hilo in due time linamachungu na kuumiza kama si kuvunja moyo. Lakini kama kiongozi, tabia ya kulalamika inaondoka unaanza kuitazama kama changamoto ambayo lazima uipatie jibu.
Nafurahi, kwasasa, kwasababu Joshua alishindwa. Kujifunza kwa kushindwa ktk uchaguzi ambapo ulikuwa na matumaini ya kushinda kunazidi kuifunua tabia kiongozi ndani ya mtu. Angekuwa mwingine angevunjika moyo na kushindwa kabisa kusimama katika zamu ya pili.
Alishindwa, akasimama tena kuingia katika mapambano mtaji wake mkubwa ukiwa ni watu wa jamii yake. Ndiyo, watu hao ndiyo:
- waliopanga naye mikakati ya kampeni
-waliomsikiliza alipohutubia
- waliomtia moyo kila alipotaka kukata tamaa
- waliotia moyo wakati wote wa kampeni
- waliokwenda kumpigia kura
- walihakikisha wanalinda kura
- waliosema pamoja naye "TUMEANZA NA MUNGU, NA TUMEMALIZA NA MUNGU" baada ya ushindi.