Lema mwanasiasa Bora wa Mwaka 2011

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
305
Ni ukweli usiopingika kuwa Godbless Lema amekuwa ni mwanasiasa mwenye kuibua mijadala mingi hapa nchini, ndani na nje ya bunge. Kwa uchache utaungana nami kukumbuka hotuba ya waziri kivuli wa mambo ya ndani aliyoitoa bungeni ilivyovuta hisia za watanzania wengi. Bila kusahau tamko lake lililopinga mwafaka uliofikiwa kati ya madiwani wa CCM na Chadema Arusha na kupelekea madiwani hao kufukuzwa Chadema.

Ni hivi majuzi tu ametoa waraka wake kuhusu kufukuzwa Kafulila unavyojadiliwa hadi leo hii. Ukiachilia mbali misukosuko yake na harakati za kuwasaidia wananchi wa jimbo lake la Arusha mjini hadi kupelekea kuwekwa rumande kwa wiki mbili, vile vile tumejulishwa Lema amepata tuzo yamwanasiasa bora na jasiri kijana kutoka blog moja nchini na kuwashinda wanasiasa wengine machachari waliotamba mwaka jana kina Zitto, January na Mnyika anayeibukia kwa sasa. Kwa vigezo hivi sina budi kabisa kusema GL amekuwa mwanasiasa bora wa Mwaka huu tunaomaliza wa 2011, nafikiri utakubaliana nami.

 
waziri mkuu anaposema uongo....naomba mwongozo
 
JF imekuwa kisiwa cha wapambe wa Lema. Kila siku watu wanaanzisha thread zinazomhusu wakati kiuhalisia hamna alichikifanya zaidi ya kuifanya Arusha kuwa uwanja wa vita.
 
Kweli Lema kiboko unakumbuka hii....

 
JF imekuwa kisiwa cha wapambe wa Lema. Kila siku watu wanaanzisha thread zinazomhusu wakati kiuhalisia hamna alichikifanya zaidi ya kuifanya Arusha kuwa uwanja wa vita.
That is all about politics
 
JF imekuwa kisiwa cha wapambe wa Lema. Kila siku watu wanaanzisha thread zinazomhusu wakati kiuhalisia hamna alichikifanya zaidi ya kuifanya Arusha kuwa uwanja wa vita.
Mkuu kwani wewe binafsi ulitalajia afanye nini zaidi ya alichokifanya?je unajua watu wa Arusha wanatarajia nini kutoka kwa mbunge wao?je mahitaji ya Jimbo la Arusha mjini ni sawa na yale majimbo ya Nyangw'ale na Igunga?ni vyema kufanya utafiti yakinifu kabla ya kutoa lawama!
 
Mi nadhani SUGU ni zaidi kwa ule uwezo wake wa kutuliza ghasia za machinga Mbeya
etc
Orodhesha vigezo ulivyotumia na tupe udhaifu wa vigezo vilivyotumiwa!ukifanya hivyo utaeleweka kiuraisi,vinginevyo itakuwa chuki binafsi!
 
JF imekuwa kisiwa cha wapambe wa Lema. Kila siku watu wanaanzisha thread zinazomhusu wakati kiuhalisia hamna alichikifanya zaidi ya kuifanya Arusha kuwa uwanja wa vita.
Ni kweli kaifanya lema Arusha kuwa uwanja wa vita kwa sababu amewaambia vijana hakuna dhambi kubwa kama uoga hivyo tusiwaogope mafisadi na vibaraka wao polisi...na kwa hilo amefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana hivyo tuna chukulia alicho kifanya Lema mwaka huu(2011) ni kututoa uoga...
 
Kweli Lema kiboko unakumbuka hii....
Asante Easyfit kwa kutukumbusha majibu ya Lema kwa Pinda alipolidanganya bunge, huu waraka nao ulijadiliwa sana. Msingi wangu mkuu wa kumkubali Lema ni jinsi hoja zake zinavyoigusa jamii, you know politics is about people, kama wewe ni mwanasiasa na uko dull no one speaks about you and your issues for good or for bad, you are as good as dead politician.
 
Kawatoa uoga? Mbona alivyojipeleka mahabusu kila mtu aliingia mitini? Unakumbuka skendo ya Mbowe kuwakimbia polisi?
Kama hii ndio unaiona ni achievement, basi upo completely wrong.

Ningemuona kafanya cha maana kama angewapa wananchi uelewa wa haki zao dhidi ya polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…