Lema jabali la siasa na Gwiji la hotuba Tanzania

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
24,199
22,646
MUNGU awe nanyi.

Wanamwelewa na anawaelewa wapiga Kura wake wanataka nini.Ukisikiliza hotuba zake huwezi kuchoka huyu huongea ndani ya mioyo ya wasikilizaji. Huyu anaishi ndani ya mioyo ya wapiga kura wake ametapakaa kama Oksijeni hashikiki hakamatiki ukilikamata jinalake unakamata wapiga KURA wake kwa kuwa anaishi ndani ya mioyo yao. si Mpangaji ni mkazi wa Kudumu

Kwenye uwanja wa mchezo wa Mpira wa Siasa usio na mbigiri na kokoto na majabali basi tegemea kufungasha magoli mengi.

Juzi Katoka likizo Mechi ya Ngarenaro kashinda wiki ijayo.Tindigani Kimandolu....nahuko nako.anakwenda kushinda.

Katika Falsafa pana za kisiasa Tunasema paka Karudi ....kule porini wanasema Simba wa Lobo ndani ya Seronera.

Huyu ni Simba wa siasa mtazame jukwaani hotuba zake hasomi karatasi huhutubia Arusha lakini Mbeya Mwanza Kagera Mara wakasikia kwa sababu watu huongea kupitia kinywa chake. Siasa ni Nguvu na Nguvu hiyo ipo kwa Wananchi

Tulijenge Taifa letu kwa mikono Mingi Siasa sio uwaduwi siasa ni Upendo Amani na Maendeleo.

Simba wa Lobo zidi kuunguruma Makambako mpaka Namanga Holili mpaka Mtukula sauti yako isikike.

MUNGU ibariki Tanzania
 
Hakuna mtu makini anayemuelewa huyo mropokaji, labda wanywa viroba.....na bahati mbaya vimepigwa marufuku sijui 2020 akina nani atamuelewa
 
Hakuna mtu makini anayemuelewa huyo mropokaji, labda wanywa viroba.....na bahati mbaya vimepigwa marufuku sijui 2020 akina nani atamuelewa
Kwa hiyo watu wa Arusha wanaomchagua wote siyo makini ! Wewe uliye makini na hunywi viroba tutajie mchango wako wa wazi kwa taifa zaidi ya kujipendekeza kwa watawala.
 
Back
Top Bottom