Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.
Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta, alisema.
Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni, aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.
Gazeti la Nipashe.

...hawachelewi kuidungua.
Chadema inapelekea watu wa Usalama wa Taifa waanze kutafuna per diem za kumfuatilia Lema mikoani. Kwa usalama wa Taifa wa hivi ni bora nchi isiwe na kitengo cha usalama wa Taifa, ni usalama wa Taifa gani una-deal na kufuatilia maandamano ya vyama huku Twiga wakisafilishwa kwa ndege kwenda nchi za nje bila kufuata taratibu? labda mimi sifahamu nini maana ya usalama wa Taifa.Tatizo la CCM ni kufanya kazi kwa matukio hawaangalii zaidi ya hapo, kuwa hili walichoangalia ni ku-neutralize furaha ya ushindi wa Arumeru Mashariki, kama walivyopiga marufuku mikutano Dodoma baada tu ya CDM jana kuitikiwa na watu. Sasa kazi inayofuata ni kuanza kumfuatilia Lema popote atakapo kwenda. Kuna wengine walifikia kusema ukimpiga teke chura unamsaidia mwendo.