kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,829
- 20,257
Rais Michel Aoun wa Lebanon ameonya kuwa, iwapo utawala haramu wa Israel utachukua hatua yoyote ya kukanyaga uhuru wa kujitawala nchi hiyo ya Kiarabu, basi ujiandae kwa jibu kali.
Bila kutoa ufafanuzi na maelezo ya kina, shirika la habari la Ruters limenukuu taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais Aoun ikiutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kufanya jambo lolote linaloweza kuhatarisha usalama wa taifa la Lebanon na kusisitiza kwamba Beirut itajibu mapigo kwa nguvu zake zote kwa chokochoko hizo.
Hata hivyo kauli ya Rais wa Lebanon inaonekana kuwa radiamali kwa matamshi yaliyotolewa Alkhamisi iliyopita na Yisrael Katz, Waziri wa Kiintelijensia ya Israel aliyesema kuwa: "Lebanon yote itateketea iwapo Hizbullah itarusha japo kombora moja Israel".
Haya yanajiri siku chache baada ya Kituo cha Utafiti cha utawala haramu wa Israel kukiri juu ya uwezo wa kijeshi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon na kueleza kuwa, uwezo wa Hizbullah uko katika kiwango cha majeshi bora ya Mashariki ya Kati.
Ikumbukwe kuwa, katika vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika miaka ya 2000 na 2006 na Hizbullah na 2014 na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, utawala huo ulishindwa vibaya na umekuwa ukikiri wazi uwezo wa kijeshi wa wanamapambano hao.
My take:Hahaaa wachapane tushachoka kutishiana nyau