Lazima uingie gharama

MBWAMBO NICHOLAUS JR

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
423
Reaction score
434
Habari ya mda huu wadau wa JF....
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada


Kwenye maisha tunayoishi aidha ulimwengu wa kimwili au kiroho lazima tujue kuna gharama zipo na lazima tuingie ili kufikia pale ambapo tunataka kufikia...

Kwenye ulimwengu wa kiroho nadhani kila mmoja anajua gharama yaaani ugumu wa kuyashika yale ya Mungu namaanisha sheria zake na maagizo yake ili siku ya mwisho tukae peponi tu-enjoy.....

Jaribu kufikiria tuuu gharama ya kujizuia kusema uongo kuzini kuiba na n.k


Haya sasa tuje huku kwenye maisha yetu ya kila siku tuuu... Angalia gharama zinazotumika


Kumbuka gharama hizi sio pesa tuu bali hata muda na akili ukiunganisha na maujuzi kama yote....

Angalia gharama yaani ile cost ambayo politician wanaingia wanaweka chambo Kwa wananchi ili tuuu waje kuchaguliwa mwisho wa siku.... unakuta mtu hata kanisani au msikitini haendi sisemi Kwa ubaya ila najaribu kukupa picha tuu jinsi watu wanavyo ingia gharama.....


Angalia kwenye Biashara watu wanaingia gharama ya matangazo ili tuu atengeneze brand yake na auze then apate faida


Hata kwenye sekta ambayo watu wengi wenye pesa na hata masikini hapa kila mtu lazima aingie gharama tuuu....

Fikiria mwanaume anavyopiga porojo kwa mwanamke ili tuuu apate PAPA...Ebu fikiria mdada wa watu pale anapoenda kwa boyfriend wake anaosha vyombo anafua nguo hii yote ili anatengeneza mazingira aje kuolewa kwa kuonekana wife material tena wadada wengine utakuta anakubali hadi kuzalishwa ili tuuu atengeneze njia ya kuja kuolewa...

But my friend kwenye aspect either Business or other issues unapotaka kuingia gharama make sure you count risk and return wajuvi wanasema PROBABILITY win game or lose game


Maisha ya siku hizi lazima ukubali kuingia gharama other wise hutofanikiwa kupata kile unapotaka

Nawakumbusha tuuu usione watu wapo na maisha mazuri hapa town kuna gharama waliingia


Usione watu wana watoto wazuri yaaani mademu wakali kuna gharama waliingia kuna cost walitumia inaweza kuwa pesa au gharama zingine za foko za hatari mipango mikubwa

Usione wachezaji wakubwa kama Messi au Ronaldo kuna gharama mpaka wamefika pale wamefanya mazoezi sana mpaka na mambo mengine ...

Kwaio better to die rather than to suffer


Karibu kwa experience ambayo uliifanya kwa gharama fulani then ukafanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ