Lawrence Masha apendekeza Mwakyembe afukuzwe Uanachama TLS

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Mkutano wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) unaendelea huku kukiwa na hamasa kubwa baada ya kuelezwa kuwa Tundu Lissu kapata dhamana na yuko mbioni kuja Arusha.

Majadiliano kadhaa yanaendelea ambapo Wakili Laurence Masha amesimama na kutoa Pendekezo kuwa Dr Harrison Mwakyembe ambaye ni mwanachama wa TLS afutiwe uanachama kutokana na kutangaza azma ya kukifuta chama chao. Wajumbe wamemshangilia kuonyesha kukubaliana na hoja yake.

Pia Mwanasheria mmoja amenusurika kutolewa baada ya kupendekeza uchaguzi uahirishwe ili kanuni zitengenezwe.

Tuendelee kufuatilia hapa kinachojiri na naamini Mods watasaidia kutoa updates endapo nitachelewa kufanya hivyo

Updates:

1650hrs: Tundu Lisu ameingia muda huu katika ukumbi wa Mkutano wa TLS hapa Arusha na kupokewa kwa shangwe
img-20170317-wa0041-jpg.482430

Lisu.jpg

Jumamosi Updates

Zoezi la upigaji kura limeanza baada ya wagombea waliosalia kujinadi.

Kura zimepigwa tayari na sasa zoezi la kuhesabu kura linaendelea. Ulinzi wa kura ni mkali sana na mchuano ni mkali sana kwa Wagombea Lisu na Wakili Francis

Matokeo yatatangazwa rasmii majira ya saa Tisa alasiri leo hii. Stay Tuned

RASMI

TUNDU LISSU ASHINDA URAIS WA TLS KWA KISHINDO
 
Mkutano wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) unaendelea huku kukiwa na hamasa kubwa baada ya kuelezwa kuwa Tundu Lissu kapata dhamana na yuko mbioni kuja Arusha.

Majadiliano kadhaa yanaendelea ambapo Wakili Laurence Masha amesimama na kutoa Pendekezo kuwa Dr Harrison Mwakyembe ambaye ni mwanachama wa TLS afutiwe uanachama kutokana na kutangaza azma ya kukifuta chama chao. Wajumbe wamemshangilia kuonyesha kukubaliana na hoja yake.

Pia Mwanasheria mmoja amenusurika kutolewa baada ya kupendekeza uchaguzi uahirishwe ili kanuni zitengenezwe.

Tuendelee kufuatilia hapa kinachojiri na naamini Mods watasaidia kutoa updates endapo nitachelewa kufanya hivyo
Huyo anayetaka uchaguzi uahirishwe ni msukule wa Mwakyembe
 
Magufuli soma alama za Nyakati... Moto unaounguza nyika huanza na moshi tu.....

Haya ya TLS, Mahakama kutupulia mbali makesi yako yasiyo na msingi... Wabunge wa chama chako kutaka kumpigia kura ya kutokua na imani na waziri mkuu wako etc ni cheche tu zinazoashiria moto!!

Vitisho na mikwara yako watu wamepuuza!!
 
Watanzania wapole ila upuuzi hawataki.
 
Wanasheria mnatakiwa muungane kuliko kipindi chochote. Nyie ndo kama defense ya mwisho mliobakia.

Msimame imara, mitikisiko mikubwa inakuja ila muwe imara kuliko wakati wowote ule.

TLS ni ya wanasheria kutoka vyama vyote vya siasa. Kazi iliyopo ni Lissu sasa kuwaunganisha wawe wamoja na kuacha tofauti zao za kiitikadi na kisiasa pembeni. This is the only way TLS will move forward.
 
Back
Top Bottom