comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Mh Rais lawama zote za kukosa ajiri nchini zinazotolewa na wahitimu mbalimbali nchini zinaelekezwa kwako, wananchi bila kujua tatizo linasababishwa na Waziri wa Utumishi, menejimenti ya umma na utawala bora, Mh Rais wananchi wamechoka na hadithi za Waziri Kairuki, Mh Rais wananchi wanakata tamaa sana kusikia matamko yasioisha na yanayojirudiarudia kutoka waziri Kairuki hakuna shaka kwamba ameshindwa kuitendea haki katika ubunifu wa Sera bora za ajira, Ajira mbadala, Mikataba na Mazingira bora ya ajira, udhibiti wa soko la ajira katika sekta binafsi katika kuweka Utanzania kwanza katika sekta ya binafsi Private Sector Employment Control Mechanism maana utakuta wageni Wahindi, Wachina, Waarabu na Wakenya wamejazana katika sekta binfasi nchini, kitu ambacho huwezi kukiona katika nchi hizo tajwa wao wanalinda soko lao la ndani la ajira nchini kwao, sasa ni wakati wa serikali kuweka mkazo ajira iwe kwa watanzania kwanza,Aidha, uthibiti wa utoaji vibali vya ajira kunakofanywa na Wizara hiyo nyeti sana katika
kukuza uchumi kupitia watumishi wa umma ndio tatizo kuu kama sio janga kuu la wazawa, watumishi wa umma na wahitimu wote wanailaumu Serikali kwa kukosa ajira kuliko vipindi vyote vilivyopita, hiyo yote inaletwa na Wizara hiyo mama sana na uti wa mgongo kwa utumishi na utawala bora nchini kwa kukosa ubunifu ili kuboresha mahusiano bora