Salaam
Wakuu naona muda upo kasi sana,na baadhi wanaachwa nyuma na muda.kisha anabaki analalama anakimiwa.kimsingi matendo yao ndo yamechangia wengi kufika hapa.
Nalusha jiwe gizani na sijui litampata nani,imefikia hatua sasa kila mmoja analalamika,anasikitika anachukizwa.kwani staki kuamini kama haya yanayotokea ya kuhusu roho za watu tuyabebeshe itikadi,mihemuko na mapenzi ili tupate jibu
Hata tukilaumiana sana na kuchukiana kimsingi haitusaidii sana.kilichopo ni kufanya malekebisho kwenye suala zima la utendaji kazi,imefika hatua kuwe na umoja wa kitaifa utaotambukika na kuamua hatma zetu,ccm na chadema hasa kwa sasa hawana hati miliki ya nchi hii.nchi hii ina hati miliki ya wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama
Inatosha sasa kwa pamoja tutafute dira ya nchi yetu.namkumbuka hayati Justine kalikawe aliwai kuimba.akiwalalamikia baba na mama yake kuwa babu na bibi yake waliwazaeni halafu wakawalea mkakua katika amani,lkn mbona sasa mnatuondolea sisi amani yetu.mwisho kunukuu.najua mauji makubwa visa vikubwa duniani vililetwa na tamaa ya wanasiasa ambao ni wanadamu baba na mama yetu.
Kwa pamoja tuchukue hatua ya kuhakikisha Tanzania yetu anabaki salama kwa ajili ya maisha ya watoto wetu kama babu na bibi walivopambana kutuacha hapa.ifike hatua mnyeti akubali Fanya kazi na wanachadema wanachadema wafanye kazi na magufuri.kama wakristo wanavofanya na waislamu halafu na hawa wote wenye dini wanavofanya na wasio na dini.mawazo tofauti yasitutenge na kila pambano lina mwisho na mshindi hupatikana na maisha nayo ni lazma yaendelee.
Tupunguze lawama na tutafute maridhiano kitaifa kisha tusonge ni kweli tunapoteza muda kwenye mambo yasiyo na msingi na yenye msingi tumeyapa kusogo.
Ni muda utakaotuambia