Land banking

Sir. Pinto

New Member
Joined
Aug 2, 2013
Posts
4
Reaction score
3
Wanajamvi, salaam. Mimi ni mdau mwenzenu kwa takribani miaka 12 sasa, naomba leo niwashirikishe jambo langu, nimekuwa na ndoto za kuwa Mwekezaji kwenye mali isiyohamishika (real estate).

Kwa mazingira yetu ya Tanzania na uchumi wetu, na kwa kuzingatia mimi ni mdau mwenye kipato cha kati na aliyejiajiri, ndoto zetu vijana daima huwa ni ndoto kubwa kubwa.

Basi, katika pita pita yangu na kutafuta maarifa kwa wale wanaofanya hizi biashara hasa wauza viwanja na majumba, mmoja akanidokezea aina ya uwekezaji ulionivutia kwa haraka sana kwenye hii mada ya mali isiyohamishika yaani (Land banking), nimejitahidi kusoma kwenye tovuti mbalimbali na vitabu kuhusu hili eneo ili kupata ufahamu wake zaidi lakini nimegundua ni eneo pana sana.

Hivyo basi, leo hii naomba kwa wenye ufahamu wa local context wanisaidie dondoo, ushauri , maoni na practical experiences kwenye namna ya kuufanya huu uwekezaji kwa mazingira ya hapa nchini kwetu Tanzania. Natanguliza shukurani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…