Lakini wazungu wanamkubali Lowassa kweli?


Watu kama wewe INNOCENT CHACHA ni wa kuogopwa kama ukoma! Sasa hao wazungu ndo akina nani kwenye mambo ya nchi yetu?

Kwani siwaligoma kutoa misaada ya kibajeti toka mwaka jana, tumekufa? Hao hao unaowaona miungu si walimsusia Rais Kenyatta, kwani wakenya walikufa, siwamekuwa even stronger!!! Wao kama hawatamtaka Laigwanani wetu wasepe tu!!! Tutakamua pesa za kodi kitaeleweka tu!! Mapato ni mengi sana ndani; tutabana uwepaji wa kodi tutatoka tu!!! Mbona tulifunga mkanda wakati wa Mwalimu... Forecast & determination ndo itatutoa kwenye hili lindi la matatizo. Laigwanani ataweza; infact he want to prove you all wrong...

Kama hawamtani wakale ndimu tu!!! Hata Pasco anajua haya.
 
Wazungu na wachina wataupokea ushindi WA lowasa kwa tahadhari wakisubiri kuona kama atasimamia maslahi yao au tofauti wakitumia msemo wao "time will tell"
 
Ukweli ni kuwa huwezi kuwa rais wa nchi yoyote ya dunia ya 3 bila kukubaliwa na Marekani na European Union

Mugabe ni rais wa dunia ya ngapi? Nitajie nchi hata moja ya ulaya iliyo na kura ya veto ambayo ina mahaba na Mugabe. Kama wazungu hawaujui muziki wa lowasa wajaribu kujiingiza ndani ya kumi nane zake waone wanavyofyatuliwa, kumbuka lowasa si mtu wa maneno ni mwanamikakati sugu yule.
 
Hii hoja nzito. Vilaza kaeni pembeni. Kuna tofauti kubwa ya nilichoandika na ulichopost.


Chacha, nina wasiwasi kuna mtu alikusaidia kuandika swali. Basimwite auk tafasiri na majibu

mzungu humpenda ----.....na lofa ....asiyejua thamani ya alicho nacho.....


Pia yule anaeamini mini kuwa ni Masikini ili hail ni Tajiri....


humpenda anayekubali kunyonywa...

hivyo kumpenda au kutompenda sio issue.....


sasa umeelewa?
 
INNO, umenikumbusha wale wenzetu niliowaita hivi!, Online Puppets: Kumbe Tunao "Puppets" Wengi Kuliko ....

kumbe na wewe ni mmoja wa kundi hili!. Kwani hao wazungu ndio nani?!.

Ni kweli Bajeti ya Tanznia ni bajeti tegemezi ya kutegemea bakuli!. Hiki ndicho the best CCM ilicholifanyia taifa hili!, kutufanya ni taifa omba omba huku tuna rasilimali lukuki!. Tanzani sio masikini, bali umasikini wote huu umesabibishwa na CCM!.

Kama wewe ni mtu wa kujikombakomba kwa wazungu, zisome pongezi zangu kwa shujaa huyu!.
Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa! Ni kweli Balozi wa Uingereza...

Pasco
 
Kweli kama huyo ni mtanzania basi wakoloni walituachia sumu mbaya!Hatumchagui mtu anayependwa na wazungu bali anayeweza kusimamia Rasilimali tulizonazo ziweze kukidhi mahitaji ya watanzania.
 
Naomba tembelea hapa
Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa!....


watu wa kujikombakomba kwa wazungu wanaona ni dili!.
P.

Wa ng'wa faza Pasco, umeniamsha sana!!!

Haya ndo niliyokuwa nayazungumzia. Eti mtu analeta hoja, hivi Lowassa atapendwa na wazungu!!! Seriously? Yaani tunaona sifa kupendwa na wazungu!

Wengi ya watu wanawaona wazungu ni watu; ukoloni umetawala ubongo wao. Mkulu wetu aliwahi hata kujisifia kuwa an aurafiki na GWB, later BHO....sikushangaa maana asili yake inamhukumu. Huyo ni historia tayari, na aende kwa amani akapumzike...tena tunamhakikishia amani tu.

Kwa kweli mabadiliko ndiyo tumaini pekee... Genge lapaswa kupumzishwa kidogo...
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…