Radhia Sweety
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 4,433
- 1,772
Kwa asilimia kubwa, nchi za dunia ya tatu zinaendesha bajeti zao kwa kutegemea misaada kutoka nchi zilizoendelea, hususani Marekani na Jumuiya ya Ulaya.
Watoa misaada hao wamekuwa wakitumia udhaifu huo wa umaskini kutengeneza urafiki wa kinafiki na vyama vya siasa vinavyoongoza nchi hizi fukara.
Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo. Tangu uhuru imekuwa ikiishi kwa misaada ya nchi za magharibi na kwa vyovyote vile nchi hizi ni wanufaika wakubwa wa rasilimali zetu. Na kwa vyovyote vile CCM imeshajitengenezea urafiki mkubwa na nchi hizi.
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, ushindani mkubwa ukiwa baina ya mgombea wa CCM(John Magufuli)na yule wa Ukawa(Edward Lowassa). Hisia nyingi mtaani ni mapenzi makubwa kwa mgombea wa Ukawa.
Lakini wazungu wanamkubali Lowassa kiasi hiki kweli? Wazungu wapo tayari kuona mabadiliko kweli?Kuna sababu gani za msingi zitakazowafanya waiondoe CCM madarakani kama zipo?
Nywele zake tu zinatosha kuwashawishi wampende....SWALI jingine?
Mods hii hoja nimeijenga kwa kutumia akili nyingi sana. Mkiifuta kizembezembe nitawafananisha sijui na kitu gani.
Kama umejenga hoja kwa "akili nyingi sana", itaonekana tu huna haja ya kuomba rehema za Moderators.
Back to the topic sasa.
Unasahau ni katika kipindi hiki cha utawala mbovu wa JK Mrisho ndipo ubadhirifu mkubwa umewahi kutokea.
Tanzania inategemea misaada, na unachopaswa kutambua hata nchi zilizo katika uchumi wa kati na baadhi ya uchumi wa juu kabisa hutegemea misaada(hiyo ndiyo dunia ilivyo). Sasa tutakuwa wapumbavu, na naomba nirudie hili, Tutakuwa wapumbavu wa hali ya juu kutumia safari za Rais eti kigezo cha kuomba msaada? Tufute kazi za mabalozi sasa, if that's the case. Yaani jumla ya safari zote zinaweza kuteglngeneza bajeti ya nchi.
Pili, kwa rasilimali zilizo nchini ni kiwango kidogo sana, narudia kiwango kidogo sana cha misaada tunachotegemea.
Hatuhitaji wazungu kudetermine fate ya watanzania. Hapa ndipo tunaposema 'Liwalo na liwe', tunahitaji watanzania kumkubali mgombea not light/white skin.
Hii hoja nzito. Vilaza kaeni pembeni. Kuna tofauti kubwa ya nilichoandika na ulichopost.
Hii hoja nzito. Vilaza kaeni pembeni. Kuna tofauti kubwa ya nilichoandika na ulichopost.
Hii hoja nzito. Vilaza kaeni mbali
Utaendekea kucopy na kupaste "vilaza kaeni pembeni", Sasa naelewa kwanini katika ule uzi mwingine umeitwa 'nyau'.
Hivi majina ya selection za UDSM yameshatoka?
Mimi ni mvumilivu kama Lowassa. Umeona nimereact kwa kuitwa nyau?
Mods hii hoja nimeijenga kwa kutumia akili nyingi sana. Mkiifuta kizembezembe nitawafananisha sijui na kitu gani.
Hii hoja nzito. Vilaza kaeni mbali