Laiti Kama Ungekuwa ni wewe ungefanyaje?

steven13

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
323
166
Habari Wakuu,

Nikiwa na rafiki yangu tumekaa In a restful place tukijadili mambo kadhaa,akanieleza kisa hiki

-Yuko kwenye mahusiano na wanawake wawili tofauti na anapata wakati mgumu katika maamuzi ya aidha kumwacha yupi ama kuwaacha wote kutokana na maswaibu haya

MWANAMKE WA KWANZA
-mwanamke huyu ni muislam na yeye ni mkristu.Alishakuwa na mahusiano na mwanamke huyu kwa miaka mingi ikiwemo kuachana na kurudiana mara nne(4) na mara zote katika kuachana jamaa amekuwa ndio mkosaji

-Jamaa anataka kufunga ndoa ya kikristu na mwanamke hayuko tayari kabisa kubadili dini na anatoka katika ukoo ambao wameshika sana dini ya kiislam.Pia wapenzi hawa hawako tayari kufunga ndoa ya kiserekali kabisa

-Jamaa anaogopa kumwacha ghafla akiwaza mara zote alizomkosea mwanamke huyu na still mwanamke akimsamehe na kurudiana nae ndani ya miaka 8 sasa


MWANAMKE WA PILI
-Wako dini moja wote ni wakristu wa dhehebu la RC

-mwanamke amemzidi mwanaume umri kwa miaka 03

-Mwanamke anampenda zaidi mwanaume in such a way jamaa anaogopa kumuacha ghafla sababu ya mpenzi wake wa kwanza(dini tofauti).

-Anaomba sana hela kuliko mwanamke wa kwanza(anapiga sana mzinga thou not Gold digger)

-Jamaa anatamani kumuacha lakini hajui atumie njia ipi itayokuwa nafuu kupunguza maumivu kwa mwanamke huyu kwani kuachwa kunauma na ubinadamu/utu wema ni silaha.Je kama ni kumwacha atumie njia ipi kumwacha kwa amani?

-mwanamke huyu anang'ang'ania jamaa amuoe haraka na mwanamke huyu ana elimu lakini hajishughulishi na kazi yoyote kwa sasa baada ya kupigwa chini kazini mwaka jana mwezi wa 8

Shughuli iko hapa,

Ungekuwa ni wewe ungefanyaje?

Ungewaacha wote?

Ungemchagua yupi na kwanini?

Je ushauri mzuri ungekuwa ni upi?

God bless you All

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wa siku hizi mna jinsia za kiume ila roho na maamuzi yakikehapo ni kwamba

asha mi nataka kuoa na nitafunga ndoa ya kikristo,

badili dini au niruhusu nitafute wa dini yangu,


umemaliza.
Mkuu si juzi tu january umekuja na thread unaomba msaada wa kiroho.

Acha mbwembwe mkuu,usikariri kila mtu anaoa kwenye umri flani.Umejuaje umri wangu

Tubaki kwenye mada,vipi kuhusu kumuumiza tena kwa mara ya tano kwa kumuacha sababu ya dini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom