Laiti kama jana ningekuwa na ka manati kangu ka kizungu hata cjui nini kingetokea

General Galadudu

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,868
2,200
Jamani nchi hii ma stress yamekuwa mengi sana hadi unaweza kujikuta unataman kufanya ambacho haukutamani kufanya..... maana tunasikia mara huyu anauza sembe mwingine unaambiwa kaitwa polisi kwenda kuhojiwa mara yule wa kutoka kolomojie anatumia vyeti vya mtu mwingine...... hatujakaa sawa tunaambiwa mtu kavamia studio na kikosi maalumu jamaa wakiwa full loaded..... eh..... nashangaa shangaa nikackia hii kali zaidi safari hii eti ukitaka kuoa lazima uwe na cheti cha kuzaliwa..... nikabaki najiuliza..... kwani hawaamini kama huyo muoaji amezaliwa?

Nikaona hapa stress za haya mambo zinazidi, nikawazaaaaaa...... nikaamua kuutafuta mchepuko wangu ambao ni njia kuu ya jamaa mmoja hivi dereva wa magari makubwa ya mizigo, tukaenda kwenye ka pub flani hivi huko huko mtaani kwao..... yeye huwa namgegedea nyumbani kwake juu ya kitanda wanacholala na mume wake na nikimaliza najifunga taulo ya mume wake naenda kuoga, sasa wakati tunapiga biere zetu huku tunatafuna kitimoto ya kuchoma, kuna jamaa mmoja hivi nilimstukia kitambo tu kuwa anafuatilia nyendo zetu na mara nyingi alikuwa anajaribu kufanya tukio baya sana ambalo lingemgharimu kama angelifanikisha....... eti alikuwa anajaribu kutupiga picha, muda wote huo nilikuwa cjamstua huyu bi mchepuko kama kuna fyatu mmoja anafuatilia nyendo zetu maana sikutaka kumstua.

Zikaletwa bia nyingine mbili na zikafunguliwa kabisa, tukaanza kunywa lakini kabla hatujamaliza nikamwambia aende toilet halafu apitilizie huko huko kwa mlango wa nyuma, hakutaka kuhoji sana maana anajua huwa nina mbinu nyingi za kijasusi, mi nikabaki pale naendelea kunywa dakika kama tano hivi baadae na mi nikatoka kwa kupitia mlango mkubwa wa mbele, sikwenda mbali nikabana sehemu flani..... ghafla nikamuona yule jamaa ametoka anaangaza angaza huku na huko, aliponikosa akadandia pikipiki lake akaondoka kwa fujo....... msichoke kufuatilia huko mbele ya story hii kuna sakata zito sana lilitokea.....
 
General Galadudu na kamanati kake ka Mungu..vipi yule tupinkele aka Albino umeweza kumuacha kweli bila madhara yeyote Yale??
 
Na mi nikaondoka kuelekea eneo la tukio, nimefika tumo chumbani tunakunywa bia za kucndikizia kabla hatujaanza migegedano huku tukichombeza na story za chinichini, wakati mwanadada amezama na story ghafla uckivu wangu wa kijasusi ukanistua nikackia hatu za watu wakitembea lakini kwa minyato ya hali ya juu sana, mara nikaona vivuli vya watu kwny pazia la dirishani, wakapita nawahesabu idadi yao walikuwa watatu, ckutaka kumstua mwanadada..... yeye anaendelea kunisimulia jambo flani mi namckiliza lakini huku najaribu kupanga mikakati ya kupangua ile ishu.

Kwa mbaaali nikawa nasikia sauti za kunong'ona kule nje, hadi muda huo mwanamke hajui chochote......... mara tukasikia kishindo cha mlango kugongwa kwa nguvu na ghadhabu kubwa..... akastuka, huku anatetemeka akauliza nani...... fungua malaya wewe na leo ndo utaijutia siku yako ya kwanza kufahamiana na mimi..... live bila chenga ilikuwa sauti ya mume wake anaunguruma kwa hasira kuu pale nje, nikaona kaishiwa nguvu akakaa chini akaanza kulia.... nikamuhurumia sana maana mimi nilijua pale lazima nitachomoka tu lakini yeye nitamuacha kwny kadhianzito, kwa mbali na mimi woga ukawa kama unanivaa lakini ckutaka kuupa nafac ya kuvuruga plan zangu za kuchomoka pale..... nikawaza weeee nikaona hapa nitumie ile mbinu ya kimapambano inaitwa 10×10= 1, nikamshika nikamkumbatia nikamwambia twende tukafungue mlango.... akastuka akabaki ananiangalia tu nadhani aliniona kama vile chizi kusema mlango ukafunguliwe wakati nje kuna dhoruba kali inatusubiri........ nikamtoa wasiwasi nikamwambie nisikilize mimi........ hapo ndo gemu lilianzia.....
 
....... tukafika sebuleni, nikaenda kufungua ule mlango lakini kwa uficho mkubwa sana hata wale jamaa pale nje hawakusikia wao walikuwa bize tu kutukana matusi mazito mazito mengine nilikuwa hata cjawahi kuyasikia tangu niumbwe nadhani jamaa alikuwa ndo anayazindua pale.... nikageuka kumuangalia mchepuko wangu analia kwa uchungu sana, nikakohoa kiaina, jamaa wakanyamaza kuongea nadhani walikuwa wanajipanga...... nikavuta pumzi nyingi kwny mapafu, nikachezea funguo za pale mlangoni kama vile ndo nafungua mlango kumbe nimeshaufungua kutambo tu, nikanyonga kile kitasa taratiiiiibu...... nikauvuta ule mlango kwa kasi na nguvu kubwa ukafunguka, hawakutarajia tukio hilo wakaparamiana kwa fujo kutaka kuingia ndani, na mi kwa kasi na nguvu ile ile nikaurudisha tena mlango kama naufunga ukambamiza jamaa mmoja usoni halafu kwa haraka sana nikaufungua tena nikamkamata yule jamaa aliyebamizwa na mlango nikamvutia ndani nikampiga kichwa kimoja matata sana nikaona kalegea anaenda chini mzimamzima, nikamcheki vzr ndo yule bwege aliyekuwa anatufuatilia tangu kule baa.

Mambo yote hayo yalitokea ndani ya sekunde chache sana, kwa hiyo nikawa nimevuruga mipango yao nikaufungua tena mlango nikamuona mwny mke anainua kipande cha spring ya gari anataka kukishusha kichwani mwangu, nikamuwahi ngumi tatu maridadi sana za chembe akaishiwa pumzi, nikamuona anajiandaa kunipiga nadhani na mpini wa jembe ule, nikamstukia nukta za mwisho kabisa anasukuma lile pigo nikalikwepa likashuka kisogoni kwa jamaa mwenye mke..... akatoa mguno mmoja tu kisha akaenda chini kimya, yule mpigaji akastuka baada ya kumshambulia mwenzie nikamkamata shingo nikamsukumia ndani nikawafungia kwa nje.

Nikatoka mbio nikapitia kwny kichochoro flani hivi, kwa mbele yangu kakatokea kajamaa kamoja kafupi kamejaa kijingajinga hivi kameshika shoka kananifuata mbio, nikasimama ghafl kakajua nimekaogopa kakaongeza spidi kunifuata..... kabla hakajanifikia mimi kwa haraka nikapiga hatua tatu ndefu kukasogelea, kakapoteza nafasi ya kuinua ile shoka..... hapo hapo nikaruka hewani nikakafyatua kichwani teke moja la form six kakayumba huku kanaachia ile shoka nilipotua chini kakaja kasi kunivamia nikakwepa kakapita vuuup nikakapiga ngumi moja kali ya shingo hadi kakainama, hapoahapo niliachia teke moja la kidevu International sana...... chali........ Mi nikajichomoa eneo lile taratibu nikavuka mitaa miwili nikaenda kuchukua gari nikaondoka, hadi muda huu cjapewa mrejesho wa kilichotokea, hapa ndo nawaza kama ingekuwa vp kama ningetembea na ka manati kangu pendwa ka kizungu..... cdhani kama na mi ningekachomoa nikaweka risasi chemba halafu nikairudisha tena kibindoni, kwa kadhia ile kwangu lazima ningeirudisha kibindoni ikiwa na upungufu wa risasi moja au zaidi.
 
Back
Top Bottom