Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu
Kwani ulaji wa nyama hata kwa binadamu ulikuwa tangu mwanzo?
Binadamu alipokosea alileta mabadiliko makubwa sana kwa viumbe vyote....!!
Ukweli ni kwamba Mungu aliwahukumu wale tu waliotenda kosa. Nyoka atatembelea tumbo na kupondwa kichwa na uzao wa mwanamke. Eva alihukumiwa kuzaa kwa uchungu, Adamu kula kwa jasho lake. Kulikuwa hamna hukumu nyingine iliotoka kwa Mungu baada ya kuwahukumu waliotenda kosa. Mungu akuwahukumu wasio na hatia.Ikiwa ni hivyo. Na ikiwa wanyama walianza kufa kabla ya kufa wanadamu or kabla ya laana ya wanadamu, Hiyo laana inawahusu nini wanyama? or Nini kilibadilika kwa wanyama hao baada ya kulaaniwa kwa wanadamu?
Mkuu uwe unasoma basi kwa makini ninachokuwa nakuandikia ....Mkuu binadamu ni Omniveras Animal anaekula vyote ie nyama, matunda, majani etc. Hivyo anaweza ku-survive kwa kula chakula chochote kati ya hivyo, hii na sawa na kusema binadamu anaweza kuishi bila ya kula nyama.
Swali langu ni kwamba, ikiwa vifo vilianza baada ya laana ya Adam na Hawa kula tunda, wale wanyama/viumbe wanaokula tu nyama (Carnivores) walikuwa wanakula nini kabla ya hiyo laana???
Ukweli ni kwamba Mungu aliwahukumu wale tu waliotenda kosa. Nyoka atatembelea tumbo na kupondwa kichwa na uzao wa mwanamke. Eva alihukumiwa kuzaa kwa uchungu, Adamu kula kwa jasho lake. Kulikuwa hamna hukumu nyingine iliotoka kwa Mungu baada ya kuwahukumu waliotenda kosa. Mungu akuwahukumu wasio na hatia.
Kabla ya kuumbwa kwa Eva, Adamu aliletewa kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani na kila mnyama wa mwituni ili awape majina na akawapa wote majina. Ina maana kulikuwa na wanyama wa kufugwa na mwituni hata kabla ya eva kuumbwa. Hivyo hamna kilichobadilika kwa wanyama wengine tofauti na nyoka baada ya kulaaniwa wanadamu.
Nasoma vizuri mkuu, may be hujalielewa swali nililokuuliza!Mkuu uwe unasoma basi kwa makini ninachokuwa nakuandikia ....
Ulimwengu ulibadilika vipi? (Ukumbuke, mada kuu inaongelea laana ya Adam na Hawa na athari zake kwa wanyama)Nilichosema mimi ni KABLA ya binadamu kuubadili ulimwengu kwa tendo lake moja tu la kutokutii,
Unaposema "huu ufahamu uliyouandika hapa ni wa baada ya hilo kosa" unamanisha nini? Jee unamanisha kabla ya hapo hakukua na wanyama waliokula nyama? ukimanisha hata chui walikula majani? or unamanisha hakukuwa na wanyama wanaokula nyama tu? Au unamanisha wanyama walikua hawali chochote?huu ufahamu uyliouandika hapa ni wa baada ya hilo kosa,je kabla ya hapo unadhani Dunia ilikuwa hivi?
Mmmh! Hapa ata sielewi, naweza kukuuliza aliumbwa ili ale nini, na nani na ushahidi wake ikawa tuengeza maswali nje na mada husika.Hata ukiangalia namna binadamu alivyoumbwa utaona hakuumbwa ii ale nyama ila kitu kingine kabisa,lakini sasa anakula....!!
Nakusoma vyema mkuu, embu ni-clarify kile ulichomanisha:
Kulaaniwa kwa Adam na hawa hakujaathiri ufaji wa wanyama wengine, wanyama walikuepo, walikua wanakufa na kuzaliwa hata kabla ya laana ya Adam na hawa.
Jee unamanisha hivyo?
Ndio hivyo
Okey.
Nakumbuka ulisema huo ni msimamo wa ki/ukiristo, mpaka hapo unamanisha mleta mada amekuja na hayo akidhani ni ukiristo, kwamba; kumbe laana ya Adam na Hawa haijaathiri lolote kwa wanyama.
But ukijaribu kusoma post za wadau humu, utaona kwamba wengi/wote ispokua wewe (Kwa wale wakiristo) wanakubali kwamba laana ya Adam na Hawa imeathiri ulimwengu kiujumla ikiwemo mfumo mzima wa maisha ya wanyama. Jee unaliongeleaje hilo?
Jee unaushahidi wowote especially wa kimaandiko (Biblia Takatifu) kuweza kusapoti huo msimamo wako? hiyo ni kwa vile inaonekana ni msimamo tofauti na wakiristo wengine.
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:29-30 haisemi wanyama wote walikula majani..badala yake inasema mimea ilitolewa kwa ajili ya chakula..hamna sehemu kwenye biblia ambapo wanyama walianza kula nyama..Mwanzo 1:21 kuna viumbe wa majini kama nyangumi wakubwa walioumbwa siku ya tano hawajatajwa kwenye Mwanzo 1:29-30, Mungu hakuwaumba ili washinde njaa mpaka baada ya laana ya wanadamu...
Mwanzo 1:24 inayozungumzia kuumbwa kwa wanyama wa kufugwa na mwituni..ni wazi wanyama hao wa mwituni walikula wenzao , kusingekuwa na haja ya kutenganisha wanyama..
Inaonekana Adamu aliwapa majina wanyama baada ya kuwaona walivyokuwa wanaishi na tabia zao..mfano 'simba' kwa tafsiri ya kiebrania ni 'katika hali ya kikatili' ..sidhani alimuita simba simba baada ya kuona anararua mimea badala yake alivyokuwa anawala wanyama wenzake...yawezekana Adamu aliwaita kwa lugha nyingine, lakini hiyo lugha ilitafsiriwa kwa kiebrania..
Mwanzo 2:17, Mungu akamuonya Adamu kutokula tunda la kati, na kuwa akifanya hivyo atakufa hakika..inaonekana Adamu alijua maana ya kufa kwani hamna sehemu kwenye biblia Adamu akimuuliza Mungu maana ya 'kifo'..asingeweza kumuuliza Mungu alichokimaanisha kwa sababu alikwishaona wanyama wanavyokufa au kuuana...
Mkuu....
Kwa context yako,Mungu ana sura kama yako?
Mkuu kifo sio adhabu ya Asam kukosea bali matokeo ya kula tunda,dhabu ni nyingine kabisa maana matokeo ya kula tunda yalikuwepo hata kabla hajakosea ....
Najaribu kufikiri kama watu wasingekuwa wanakufa toka kipindi cha Adam na Hawa. sijui kama kungekuwa hata na nafasi ya kugeuza shingo
adam na hawa walimilikishwa dunia na viumbe vyote..baada ya wao kula tunda(kufanya mapenzi)ndipo balaa la laana lilipokuja sababu alijua idadi ya watu itaongezeka kuliko rasilimali zilizopo lkn km wasingefanya wangebaki wao peke yao milele
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
1 Mwanzo 1 :26
Mbona Umeenda Tofauti na Andiko
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
1 Mwanzo 1 :26
👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆
Nadhani Yeye Mwenyewe Amesema Hapo Juu.......... kwahiyo Kwa Uelewa Wangu Ni YES
Sasa Sijui Kama Kuna Ukanushi wa Hilo Andiko.. Na Kama Kuna Sehemu Nimefanana Na Kiumb Kingine
mwanadamu hakuumbwa ili afe..bila shaka mmeikuta jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.
Adam na hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.
Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..
Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..
Swali kuu ni kwamba je, baada ya adam na hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?
Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?
Najua jf naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.
Nawatakia jumapili njema.
ukifananisha mungu na mtu au kitu...hutaipata maana ya mungu....ni zaidi ya umoja na wingi...akili za mwanadamu haziwezi.............wakuu, ni kwa nini hapo umetumika umoja na wingi? Ni miungu wangapi waliumba mtu? Mungu "akasema" ..halafu...na "tufanye"!!!inakuwaje hapo jamani?