storyteller
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 1,544
- 1,874
Mungu Hana mwanzo wala mwisho,na huwezi kutumia akili za kibinadamu isipokuwa akupe Ufunuo Yeye mwenyewe.
Mungu Hana mwanzo wala mwisho,na huwezi kutumia akili za kibinadamu isipokuwa akupe Ufunuo Yeye mwenyewe.
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.
Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.
Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..
Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..
Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?
Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?
Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.
Nawatakia Jumapili njema.
Umewahi kujiuliza laana ni nini na kinyume cha laana ni baraka?? Unaweza barikiwa wewe na mambo yote au watu wote wanaokuhusu wakaingia ndani ya hiyo baraka, kimsingi hiyo laana ya adam na hawa iliathiri mpaka mambo yote ambayo lazima tu angekuwa na ushirika nayo, kuanzia ardhi na vyote vilivyotegemeka kwayo, mana yake chochote ambacho adam na hawa wangefikilia au kutengeneza tayali kilikuwa hakina ukamilifu tena.... jiulize kwa hii sayansi na tekn binadam ana uwezo wa kutengeneza kitu cha kudumu milele...
Kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa MFANO WAKE. viumbe wengine waliumbwa pasipo mfano wake. Maana ya mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa mungu si kufanaa sura, bali utashi na kuishi milele. Baada ya kula lile tunda Mungu alifuta kalama ya kufanana naye kwa wanadamu. Ndio sababu wanadamu wanakufa kama viumbe wengine ambao hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu
Adam na Hawa (binadamu) v. Viumbe wengine (living organisms) ni nani or kipi kiliumbwa mwanzo?
viumbe vingine viliumbwa kwanza, baadae Adam na hatimae Hawa
Bila shaka mmeikuta Jumapili mkiwa salama wana jamvi wote.
Adam na Hawa walikula tunda la mti ulokatazwa na mwenyez Mungu hivyo binadamu akapewa adhabu ya kifo.
Leo nimekuta mdudu kafa, katika mazingira hayo haionyeshi kama amekanyagwa wala kuangukiwa na kitu. Kwakua mimi si mwanasayansi nikashindwa kugundua yawezekana alipuliziwa sumu..
Imenifanya nifikiri sana kuhusu vifo vya wadudu, wanyama, miti, majani na viumbe vingine hai ambavyo vinazaliwa na kufa kwa mazingira yoyote yale..
Swali kuu ni kwamba je, baada ya Adam na Hawa kula lile tunda, laana iliyotolewa iliwalenga 'viumbe hai wote' au ni kwa 'binadamu' tu?
Kama adhabu ile ni kwa wanadamu tu, kwanini viumbe vingine vinakufa?
Najua JF naweza kupata mwanga na majibu ya kuridhisha.
Nawatakia Jumapili njema.
Najaribu kufikiri kama watu wasingekuwa wanakufa toka kipindi cha Adam na Hawa. sijui kama kungekuwa hata na nafasi ya kugeuza shingo