All in all,
Uwepo wa Mwakalinga kwenye uchaguzi wa mwaka huu umeleta changamoto nzuri. Bila kujali matokeo, nampongeza Mwakalinga kwa kujitosa kinyang'anyiro hiki. Nina sababu
1. Mara nyingi wanaogombea Kyela hutoka koo za Kichifu; kwa Mwakalinga na wengine kujitokeza kunavunja mwiko huo
2. Kwa kuwa kila mtu alito hoja na mawazo ya jinsi ya kuendeleza Kyela, naamini hata Dokta akipita atakuwa amecopy baddhi ya mbinu za kuleta maendeleo, badala ya kusubiri mgao toka serikali kuu. Mfano wa haya tumeyaona wilayani Karatu kwa Raisi wetu Mtarajiwa Dk Slaa!
3. Umetoa mwanya kwa wananchi kuelewa umuhimu wa kupiga kura. Kwamba hawatapiga tena kura bila kuhoji uwezo na sababu zinazowasukuma wagobea kutaka ubunge wa wilaya yao
4.Mwakalinga amekubali yaishe, na nashangaa kwanini watu bado wanadhani Mwakalinga ana Kinyongo. Huu ndio ushindani.
Kwa hiyo, vyovyote vile isemavyo, iwe Mwakalinga ametumwa, au amejituma mwenyewe, tumejifunza mengi hapa.
Pia naamini Mwakalinga atakuwa ameelewa sababu za kushindwa kwake. Mimi nimeona haya
1. Mwakalinga ameingia kwenye kampeni kipindi kibaya. Kipindi ambacho watu wengi walishaaminishwa kwamba Mwakyembe anahujumiwa. Binafsi nilijaribu kumzuia George kuvuta subira, lakini bahati mbaya wafuasi wa George walikuwa si watafiti wa siasa za kule kiasi kwamba walikuwa wana mpa George wrong information ( bila kujua). Kwa kufanya hivyo wamesaidia kuanguka kwa mtu ambaye naamini kabisa bado ni potential. Kwa kuwa wengi tuko mbali na jimbo hili, tulishindwa kupata hoja za msingi kumjenga George ili ajitose lini na kwa namna gani.
Kuna wakati ilikuwa ukiwauliza washauri wa George mantiki, mikakati, nk, jamaa walikuwa wanajibu mkato, hawakupi muda wa kufikiri, na in short wanakuambia wewe ni msaliti. Hii haifai. Kumsaidia mtu ni pamoja na kumuuliza maswali hata ya ndani kabisa ili unapotoa mchango wako uwe na hoja za kushawishi watu. Naamini safari nyingine Mwakalinga artakuja na mbinu mpya na kushinda
2. Kutokuwa karibu mara nyingi Kyela. Kwa kuwa George alikuwa na mipango ya kuingia kwenye siasa, ilikuwa ni vyema akajenga ukaribu na watu wa jamii zote na rika zote na kabila zote. Kyela si ya Wanyakusa: Kyela ni Metro sasa hivi. Sasa unapoanguka hata kijiji ulikozaliwa hilo ndilo jibu lake. Kwamba hata ndugu wanakuwa hawakuelewi ( na sio hawakupendi). Ukiwa ni mwanasiasa, basi ni lazima unywe na watu kwa level zao ili wajue wewe ni mmoja wao. Vinginevyo watakuita unaringa; na wewe utawaita wana wivu. Yote haya ndio huleta negative results.
Bila shaka hili George ameliona
3.Kuchagua kwa usahihi Campaign Mangers. Wapambe si lazima wawe ndugu. Ukiweka ndugu wengi kwenye kampeni zako ni kwamba watu hawakuelewi, maana watadhani mmekuja kutangaza uchifu tu. Na zaidi ni kwamba huwa arogant kwa watu , na wewe utashindwa kuwakemea kwaw sababu ni ndugu! Nadhani hili litarekebika baadaye, come 2010
Mwisho:
Nimesikia fununu kwamba kuna watu wanamkatisha tamaa Mwakalinga ili asirudie tena mambo ya siasa. Nakusihi usiwasikilize. Kajipange, rekebisha kasor njoo 2010. Au bado kuna vyama vingine na jaribu huko ili uzidi kuleta changamoto kwenye siasa za jimbo ambalo naamini una mapenzi nalo kabisa. Unaonaje ujaribu kwa tiketi ya CHADEMA ?
Pia, Dr Mwakyembe, umesikia yote, chagua yaliyo postive kutoka kwa Mwakalinga, Rhoda, Elias nk ili kama kweli wote lengo lenu lilikuwa moja, mlete maerndeleo Kyela.
Vunjeni makambi yanayomsaidia Lowasa na Makuwadi wake, tusemezane tuijenge Kyela
Mwaibisheni Mwakipesile , ajifunze kwamba anwahujumu Kyela, kule kwenye Masyeto yake, kwa faida ya watu ambao hawana uchungu na wala hwana mjukuu pale Kyela. Shikaneni mikono na Mwakalinga, na TUANZE UKURASA MPYA
TABIA ya upambe si tabia ya wana Kyela, stop being used, you are killing your own people and the Generation there after. After all, we die so soon, so why the Lowasas, and the Aziz want to use you guys? We are grown up buds......