Kwenye Mifuko ya Plastic kuna Siasa

Kwenye Mifuko ya Plastic kuna Siasa

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
2,989
Reaction score
4,163
Nchi zenye mifumo ya kijamaa ya chini chini ni tabu sana.
Wakati viongozi wa kisiasa wakitafuta kila aina ya fursa kujitajirisha pasipo kuonekana wanaiba pesa za umma.
Wamekuja na mbinu nyingine ya kujitajirisha, sasa ni kukomesha mifuko ya plastic. Hatua hii imekuja ghafla sana, tena haraka haraka na mikwara mingi. Wanaelewa kabisa kuna lundo la pesa zimewekezwa kwenye biashara hiyo kama ilivyokuwa kwenye pombe za viroba.

Nina wasiwasi kuwa hawa wanasiasa wamejiagizia huko nje contenna nyingi za mifuko mbadala sasa wamebuni mbinu za kuiuza haraka.
Serikali wanajua viwanda vinavyotengeneza hiyo mifuko, wangevitoza faini kubwa ili viache kutengeneza, mifuko inayoagizwa toka nje ya nchi ingetozwa kodi kubwa ili ku compensate gharama za uharibifu wa mazingira.
Kama issue ingekuwa ni plastic, mbina bidhaa karibu zote zinazoingizwa nchini zimekuwa packed kwenye nailon, tena uchafu wa haya mavifungashio ni mkubwa kuliko hata wa mifuko.
Kwa dunia ya leo ni ngumu sana kuepuka plastic, serikali ingebuni au kuwekeza kwenye mashine za ku recycle kuliko kuzuia.
Mtu unatembea njiani ukakutana na matunda au mboga unataka ubebe hukujiandaa na vikabu au mifuko hiyo mbadala, ina maana utaacha kununua hizo bidhaa?
Hawa wanasiasa wanachotaka ni hiyo mifuko yao iliyododa bandarini ianze kutembea, lakini ni wanafiki kuzuia mifuko na kuruhusu vifungashio.
Viwanda vya Bahresa, Mo dewji na Sayona bila kusahau Coca cola na Pepsi ndo viwanda vikubwa vinavyoongoza kwa kuchafua nchi na vifungashio vyao. Chupa zao za plastic zinaweza kuwa recycled lakini yale ma nailoni wanayofungashia chupa zao ndo tatizo kubwa.
Hawa wangebanwa hata kulipia gharama za kusafisha nchi kutokana na plastic wanazozalisha.
Hivi umekutana na bidhaa njiani kama nyama na samaki utabebea kwenye sufuria?
Kwa hiyo Makamba, nikitaka kununua mboga njiani ninunue pia na sufuria la kubebea....
 
Mbona vifingashio wanna viricycle pia,
 
Akili za kiufipa ufipa bhana ety mifumo ya kijamaa ya chini chini.Nchi zenye mifumo imara ya kibepari zimepiga marufuku mifuko ya plastic kitambo na nchi zinazotumia hiyo mifuko huihifazi na kupeleka nchi za afrika na asia kutupa yaani kifupi ni kwamba hakuna cycling ya hizo plastic bags zinakaa hadi miaka 400.Alafu misukule ya ufipa inapinga katazo la mifuko ya plastic ili watanzania wafe kwa sumu zinazo patokana kwenye uteketezaji na cancer zinazo sababishwa na nylon.
 
Back
Top Bottom