Kwenye mafiga matatu mawili yakitolewa lililobaki linaweza kupika??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye mafiga matatu mawili yakitolewa lililobaki linaweza kupika???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kizito, Mar 9, 2008.

 1. K

  Kizito Member

  #1
  Mar 9, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnakumbuka JK anakikundi anachokiita wanamtandao ingawa kikundi hicho sio Rasmi lakini kinajulikana kipo, navingozi wa kikudi hicho ni JK mwenyewe,EL na Rostam Aziz(RA). sasa tunajua yaliyompata EL na RA na kwa vyovyote vile hawawezi kuendelea na uongozi wa WAnamtandao na hapo ndipo linapobaki Figa moja!! litapikaje? Hivi kweli JK anaweza kufika 2010 bila wasaidizi wake katika harakati za wanamtandao kuwepo? mbona kwa mtindo huu anaoneka tayali ameshashindwa!

  Na tena wanamtandao wenzie wameharibu nchi haingii akilini kuwa hawakumwambia chochote kuhusu Richmond kwa vyovyote vile walimgusia, sasa alitoa hoja gani? inawezekana Akina Mwakyembe hawakutaka tu kumuomba JK nae apime uzito wa maneno uliomo ndani ya ripoti ya kamati na kuchukua uamuzi atakaoona unafaa. Wanamtandao wenzie wamekoroga nchi yeye vipi hawezi kupima uzito wa maneno akachukua uamuzi??
   
Loading...