Kwenye hili la sukari Rais wangu sikuungi mkono, uchumi ni kanuni siyo amri!

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,061
Ni dhahiri kumekuwa na mayowe mengi ya walalahoi na kuishi hai wakishangilia kauli ya Mhe. Rais Magufuli juu ya kuvamia magodown ya wafanyabiashara na kutaifisha sukari ya wafanyabiashara ili kushinikiza uimara wa soko.

Kwangu mimi hii ni sawa na kukata miti kwenye chanzo cha chemichemi kwa madai kwamba miti hiyo haitoi mchango wa maji ya kutosha katika mkondo wa maji. Mimi nadhani kwa busara zaidi mtaalamu wa mazingira angehitaji aidha kupanda miti zaidi au kuongeza mbolea, dawa na usimamizi kwa miti iliyopo ili mkondo wa maji uzidi kukua.

Sasa najiuliza, ni nini mantiki ya haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa serikali ya awamu ya tano. Mwalimu wangu wa falsafa alikuwa anapenda kunena yafuatayo:
"Waafrika wengi ni wabobezi kutibu dalili za ugonjwa na siyo ugonjwa wenyewe".

Nani haelewi hali ya uchumi wa nchi hii sasa hivi? Nani hajayaona mabonde makubwa yenye rutuba inayoweza kutumika kuzalisha mazao mengi ikiwamo miwa na kulitatua tatizo la upungufu wa sukari kwa kanuni ya kiuchumi badala ya amri?

Nani hajui kwamba wakulima wetu wanalima kimazoea pasipo kufuata utalaamu wowote huku somo la kilimo likipewa kisogo mashuleni na vyuoni?
Sasa kama hali iko hivi, utakapomaliza kupokonya sukari ya wafanya biashara utapokonya nini tena?

Biashara ya sukari ni kama biashara nyingine wala hauhitaji nguvu bali maarifa-

CONSIDER SUPPLY AND DEMAND AS YOUR PROSPECTIVE TOOL TO CONTROL YOUR MARKET.

Siamini kama Tanzania ya viwanda uliyotuahidi ni hii ya kupokonyana sukari, tengeneza misingi imara itakayowakomboa wakulima, vijana wasaka ajira na wawekezaji kwa ujumla.

Katika hili nimeamua kufuata njia ya Mark Twain kwamba 'uzalendo siyo kuiunga serikali kila wakati bali kuiunga mkono nchi kila wakati na kuiunga mkono serikali pale inapostahili tu'.
 
Ni dhahiri kumekuwa na mayowe mengi ya walalahoi na kuishi hai wakishangilia kauli ya Mhe. Rais Magufuli juu ya kuvamia magodown ya wafanyabiashara na kutaifisha sukari ya wafanyabiashara ili kushinikiza uimara wa soko.
Kwangu mimi hii ni sawa na kukata miti kwenye chanzo cha chemichemi kwa madai kwamba miti hiyo haitoi mchango wa maji ya kutosha katika mkondo wa maji. Mimi nadhani kwa busara zaidi mtaalamu wa mazingira angehitaji aidha kupanda miti zaidi au kuongeza mbolea, dawa na usimamizi kwa miti iliyopo ili mkondo wa maji uzidi kukua.
Sasa najiuliza, ni nini mantiki ya haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa serikali ya awamu ya tano. Mwalimu wangu wa falsafa alikuwa anapenda kunena yafuatayo:
"Waafrika wengi ni wabobezi kutibu dalili za ugonjwa na siyo ugonjwa wenyewe".
Nani haelewi hali ya uchumi wa nchi hii sasa hivi? Nani hajayaona mabonde makubwa yenye rutuba inayoweza kutumika kuzalisha mazao mengi ikiwamo miwa na kulitatua tatizo la upungufu wa sukari kwa kanuni ya kiuchumi badala ya amri?
Nani hajui kwamba wakulima wetu wanalima kimazoea pasipo kufuata utalaamu wowote huku somo la kilimo likipewa kisogo mashuleni na vyuoni?
Sasa kama hali iko hivi, utakapomaliza kupokonya sukari ya wafanya biashara utapokonya nini tena?
Biashara ya sukari ni kama biashara nyingine wala hauhitaji nguvu bali maarifa- CONSIDER SUPPLY AND DEMAND AS YOUR PROSPECTIVE TOOL TO CONTROL YOUR MARKET.

Mkuu wanazani uchumi ni sawa na kubreak Hydrogen and Oxygen bond.Hata kama haujui watafute wataalam wa uchumi.Kwa sababu huwez kujua kila kitu.Na wataalam wapo na wanalipwa handsomely salary mwisho wa mwezi.Where are we heading?Can someone tell me.
 
MTU hawezi ifanyia kiburi serili hata kidogo, KUWA kiongozi ni lazima KILA mwananchi aiheshimu serikali... Hapa duniani hakuna MTU yeyote mwenye kuweza ichezea serikali ....mfano mzuri ni north Korea ambapo inauchumi mzuri sana kutokana na aina ya uongozi uliopo madarakani!! Hao walioficha sukari ni zaidi ya wakatili!!! Hawastahili hata kuuona ufalme wa MUNGU!!!
Na ili uchumi wa NCHI ukue ni lazima NCHI husika izuie bidhaa kutoka NCHI za nje!!
 
Sikatai, huoni kama kuna hujuma, uchumi utakuwaje tukiendeleza hujuma,na kucheleweshana kupata hizi services tatizo lenu mna substitute uhai wa binadamu kwa tamaa za utajiri. Na serikari yenye kujali watu wake mmojammoja haiwezi kukubali hili
 
Ni dhahiri kumekuwa na mayowe mengi ya walalahoi na kuishi hai wakishangilia kauli ya Mhe. Rais Magufuli juu ya kuvamia magodown ya wafanyabiashara na kutaifisha sukari ya wafanyabiashara ili kushinikiza uimara wa soko.
Kwangu mimi hii ni sawa na kukata miti kwenye chanzo cha chemichemi kwa madai kwamba miti hiyo haitoi mchango wa maji ya kutosha katika mkondo wa maji. Mimi nadhani kwa busara zaidi mtaalamu wa mazingira angehitaji aidha kupanda miti zaidi au kuongeza mbolea, dawa na usimamizi kwa miti iliyopo ili mkondo wa maji uzidi kukua.
Sasa najiuliza, ni nini mantiki ya haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa serikali ya awamu ya tano. Mwalimu wangu wa falsafa alikuwa anapenda kunena yafuatayo:
"Waafrika wengi ni wabobezi kutibu dalili za ugonjwa na siyo ugonjwa wenyewe".
Nani haelewi hali ya uchumi wa nchi hii sasa hivi? Nani hajayaona mabonde makubwa yenye rutuba inayoweza kutumika kuzalisha mazao mengi ikiwamo miwa na kulitatua tatizo la upungufu wa sukari kwa kanuni ya kiuchumi badala ya amri?
Nani hajui kwamba wakulima wetu wanalima kimazoea pasipo kufuata utalaamu wowote huku somo la kilimo likipewa kisogo mashuleni na vyuoni?
Sasa kama hali iko hivi, utakapomaliza kupokonya sukari ya wafanya biashara utapokonya nini tena?
Biashara ya sukari ni kama biashara nyingine wala hauhitaji nguvu bali maarifa- CONSIDER SUPPLY AND DEMAND AS YOUR PROSPECTIVE TOOL TO CONTROL YOUR MARKET.
Siamini kama Tanzania ya viwanda uliyotuahidi ni hii ya kupokonyana sukari, tengeneza misingi imara itakayowakomboa wakulima, vijana wasaka ajira na wawekezaji kwa ujumla.
Katika hili nimeamua kufuata njia ya Mark Twain kwamba 'uzalendo siyo kuiunga serikali kila wakati bali kuiunga mkono nchi kila wakati na kuiunga mkono serikali pale inapostahili tu'.
asante,kwa elimu hii!
:) naipenda tanzania,siipendi serikali ya chama cha mapinduzi :)
 
Bila government intervetion kweny mixed economy wafanyabiashara wanauwezo wa kununua bidhaa nying wakaweka ndan bila ya kuziuza na wasipoziuza zitaadimika sokoni na pia zikiadimika itasababisha bei kupanda ghafla so bila serikali kuingilia itasababisha black market kutokea na hatima hali ya kiuchumi na mlipuko wa bei(inflation) vinaweza kutokea.. so ukirud kweny point ya rais leo ilkua ni vyema kwend kimkakati wa policy na vitendo kuondoa tatzo la sukari lkn mhe ametumia mamlaka ku declare war na wahujum uchumi kwa njia ya kuficha sukari. Kiuchumi naungana na raisi kipinga uhujum uchumi wa njia jii
 
nafikiri na nyama ikipanda bei, wafugaji wote wajiandae tutachukua mifugo kutoka kwenye maranchi yao na kugawa nyama bure wananchi wapuguziwe wapunguziwe ugumu wa maisha?

Swala hili alitakiwa kabla hajafungia sukari ilitakiwa aangalie upungufu uliopo halafu wakae chini na wenye viwanda waangalie wanalitatua vipi hilo suala la upungufu wa sukari na kulitatua halafu ndiyo wangefuta vibali
 
Sikatai, huoni kama kuna hujuma, uchumi utakuwaje tukiendeleza hujuma,na kucheleweshana kupata hizi services tatizo lenu mna substitute uhai wa binadamu kwa tamaa za utajiri. Na serikari yenye kujali watu wake mmojammoja haiwezi kukubali hili
There is no lifestyle of one man to feed the neighbor , kama hali ya Watanzania wenye dhahabu,ardhi yenye rutuba, mbuga za wanyama na karibia kila kitu zingekua zinaendana na uhalisia wa rasilimali gawanya kwa idadi ya watu basi utagundua kwamba kwa thamani ya shilingi yetu elfu tatu ya kununua kilo moja ya sukari siyo kubwa.
Tatizo ni kwamba raia hawana hela hivyo miundombinu mbadala ya kubadili hali inahitajika badala kulazimisha kisicholazimika.
Rais amesema serikali inafanya mkakati wa kuagiza sukari nje ya nchi ku counter attack wafanyabiashara wa ndani, umejiuliza ni mkakati gani wa serikali kuwekeza katika kilimo cha miwa kwa miaka ijayo?
 
Jamaa kila akiongea Masuala ya uchumi anazidi kuharibu! Inawezekana ikakiongezea umaarufu Yeye na Ccm yetu kwa kama ZANU PF ilivyoipoteza MDC ya Morgan Tshangirai lakin uchumi ukaanguka vibaya!
Huenda utawala wa Jakaya kny uchumi ukawa na nafuu kuliko huu!
 
Back
Top Bottom