Kwenye elimu, TAMISEMI wanateleza

Jimmy George

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
1,733
Reaction score
1,650
"Tunawaletea walimu shuleni kwenu kwa kulingana na idadi ya wanafunzi" Kauli hii hutolewa na viongozi wa TAMISEMI.

Habari zenu ndugu zangu!!
Kuajiri walimu kulingana na idadi ya wanafunzi kuna ulakini kwenye hili,mfano shule yenye wanafunzi zaidi ya 500 inakuwa na walimu 6 na mwalimu mmoja kufundisha madarasa yote.

Wakati wa kusahisha mwalimu akifundisha madarasa yote hujikuta anasahisha madaftari 233{darasa la III=56,darasa la IV=78,Darasa la V-VII=99}

Je, kuna tofauti gani na yule mwenye jumla ya watoto 1000 na shuleni kuna walimu 24 na mwalimu mmoja kuwa na masomo mawili kusahisha daftari 200 ?
 
Shule zinatofautiana, kisimiri ina wanafunzi 1100+ halafu walimu 60+ wengine wana mkondo mmoja tu unakuta mwalimu anafundisha history form C tu,full bata.
Lakini kuna shule zina wanafunzi 1000 lakini walimu wachache hii yawezekana inasababishwa na ufaulu wa shule husika,kama shule inafaulu vizuri ni rahisi kupewa walimu wengi.
Ushauri:shule zote zipewe walimu wa kutosha japo kwa wastani wa 1:25
 
Nyinyi si ndio mnaenda kusimamia kura na kwenda kwenye maandamano na ma hotuba ya watajaza wenyeweee? Subiri 2020.
 
Daaaa kuna tofauti kubwa sana
 
Niliwashangaa,nimewashangaa pale walipoamua kupeleka walimu wa sekondari msingi,kisa eti wa arts wamejaa,
hivi hawajui form one kila mwaka watoto wanaongezeka,walimu,wanastaafu,wanakufa,wanabadili kazi na mengine meengi.
Siku darasa la kwanza ya 2016 wakiingia form onr sijui itakuaje,watahamisha tena msingi kwenda sekondari?
 
Nadhani yote haya lengo ni moja kukimbia jukumu la kuajiri walimu walio mtaani kutoka 2015-2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…