kweli sisi ni twiga ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,205
4,403
KWELI SISI NI TWIGA.

1)ni sa sita usiku,balaa litapozuka.
Tukichinjwa kama kuku,na wenyewe tukicheka.
Na vichwani twa viduku,na bongo za tetemeka.
Hivi kweli sisi twiga,ama tunaiga iga.

2)tunajipanga foleni,vilonga vimezimika.
Japo wengi twahuzuni,twaogopa kusikika.
Na gari karandingani,tunahofu kufungika.
Hivi kweli sisi twiga,ama tunaigaiga.

3)na kodi zililipiwa,wapo walifaidika.
Kama walificha miwa,hili hawatoshituka.
Sisemi tumeonewa,nisije nikategeka.
Hivi kweli sisi twiga,ama tunaiga iga.

4)huo mtoko wa nguvu,nadhani naeleweka.
Wagombea sasa nyavu,punde mtanawirika.
Nyinyi moto siyo jivu,karibia mtawaka.
Hivi kweli sisi twiga,ama tunaigaiga.

5)haya tukale majani,mili izidi pasuka.
Ipauke na usoni,wao wazidi kucheka.
Tumemuweza fulani,kimoyo wafurahika.
Hivi kweli sisi twiga,ama tunaiga iga.

6)pupa pu pu ti ti ti pu,mlio unalipuka.
Shabaha yatibu jipu,haliwezi kupasuka.
Tiba ndiyo ni upupu,hapana funika shuka.
Hivi kweli sisi twiga,ama tunaigaiga.

Shairi:KWELI SISI NI TWIGA.
Mtunzi:Idd Ningawa wa Tengeru Arusha.
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160.
 
Back
Top Bottom