Kweli Lowassa tishio, tangaza nia

Kweli Lowassa tishio, tangaza nia

Joined
Jan 19, 2015
Posts
16
Reaction score
3
Dhoruba imetulia, nuru imetamalaki
Sasa naishika njia, naja tokea Kowak
Ombi ninakuletea, baba naomba nilaki
Simama tangaza nia, taifa lakuhitaji

Elimu yadidimia, kwa kasi iso kifani
Usipotangaza nia, wataizika shimoni
Ujinga utarejea, turudishwe utumwani
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hatunae kama wewe, kunako uchapakazi
Katu hauna kiwewe, ufanyapo maamuzi
Iwe Tanga ama Kawe, baba huna ubaguzi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Uchumi utachipua, kwani u mchapakazi
Milango utafungua, ajira zikae wazi
Panya rodi watanywea, tuupate usingizi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Japo orodha ni ndefu, Lushoto hadi Sikonge
Kwako hawafui dafu, wengine wasaka tonge
Uliza hata Shekifu, wamedoda ka chuchunge
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hakika wewe ni bora, bara hata visiwani
Tena umetia fora, tangu kura za maoni
Utaibuka kinara, shamba na hata mijini
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Siwezi fika tamati, pasi hili angalizo
Lifike kwenye kamati, isijeleta mchezo
Tutaipiga manati, tukimkosa tulizo
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji


Max Mondu
mondu87@gmail.com

NAWASILISHA KAMA NILIVOIPOEA.
 
Dhoruba imetulia, nuru imetamalaki
Sasa naishika njia, naja tokea Kowak
Ombi ninakuletea, baba naomba nilaki
Simama tangaza nia, taifa lakuhitaji

Elimu yadidimia, kwa kasi iso kifani
Usipotangaza nia, wataizika shimoni
Ujinga utarejea, turudishwe utumwani
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hatunae kama wewe, kunako uchapakazi
Katu hauna kiwewe, ufanyapo maamuzi
Iwe Tanga ama Kawe, baba huna ubaguzi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Uchumi utachipua, kwani u mchapakazi
Milango utafungua, ajira zikae wazi
Panya rodi watanywea, tuupate usingizi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Japo orodha ni ndefu, Lushoto hadi Sikonge
Kwako hawafui dafu, wengine wasaka tonge
Uliza hata Shekifu, wamedoda ka chuchunge
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hakika wewe ni bora, bara hata visiwani
Tena umetia fora, tangu kura za maoni
Utaibuka kinara, shamba na hata mijini
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Siwezi fika tamati, pasi hili angalizo
Lifike kwenye kamati, isijeleta mchezo
Tutaipiga manati, tukimkosa tulizo
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji


Max Mondu
mondu87@gmail.com

NAWASILISHA KAMA NILIVOIPOEA.

Amekusikia atatii kiu ya watanzania nichaguo lao
 
mtunga shairi hajielewi, sio kila ndio ina ndio kundani kuna ndio zinngine zinaambatana na utani JICHUNGUZEE WEWE WATANZANIA ANNGALIENI MSIJE MKABEBESHWA UJAUZITO MWISHO MZAE BUNDI, HAWA WATU WATOKA ZIZI MOJA SO WANAHARUFU YA UOZO KAMA HAWA WALIVYOOZA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom