Kweli Dhambi ya Zinaa Adhabu yake ina anzia hapahapa Duniani !!!

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,530
Ndugu wanajamvi kama kichwa kinavyojieleza naomba tusome kisa hiki kwa pamoja

Kuna Binti mmoja aliyelelewa katika Familia ya Dini asema alipofika Sekondari ikawa kuna Kijana anamfuata fuata tena anamuita kwa jina lake! Asema nikawa simtizami wala simuitikii hali ikaendelea hivyo.

Mara Kijana akawa anampigia simu Mara kwa Mara asema sijui hata nani aliyempa namba ya simu yangu Simu ikawa inaita sipokei Mara Shaytwan akaanza kumshawishi kichwani kwake kana kwamba anamwambia ! Si umsikilize ataka nini labda ukimwambia asikusumbue hatakuwa akikusumbua tena.

Binti akaanza kupokea simu za Kijana ,Kijana akaanza kumtongoza na kumwambia maneno laini kuwa lengo langu nataka nikuoe sitaki tufanye madhambi asema Binti Nikamuamini ikawa naongea nae kwa Simu kwa masaa kadhaa kila siku.

Daima Yule kijana akawa anamwambia binti wa watu nkishakuoa tutafanya hivi na vile akawa anapanga na Binti mambo mbalimbali ya baadae katika Maisha yao Binti ikawa Ana amini hicho anacho ambiwa!!!

Siku moja kijana akiwa na Gari yake akakutana na Binti njiani akamwambia panda nikakushushe kwenu!! Binti akakataa akambembeleza mwisho Binti akakubari kupanda gari ...

Ikawa anakutana nae njiani anampandisha kwenye Gari kisha anamzungusha alafu mwisho anamrudisha kwao binti akawa ameshazoea hali hiyo.

Siku moja kijana akamwambia Binti nimekodisha Nyumba ambayo tutaishi pindi ntakapo kuoa twende ukaione binti akakataa, Kijana akamwambia mm nataka kujua tu Je utaipenda? Mwisho binti akakubari kwenda kuiona nyumba hiyo.

Walipofika Jamaa akaanza kumshawishi binti wafanye tendo la ndoa akambembeleza kwa kumwambia maneno matamu mpaka msichana wa watu akakubali wakafanya mapenzi kwa mara ya kwanza

Binti walipo maliza akawa anajuta haamini kweli ni yeye ambaye ameangukia kwenye zinaa anasema nkarudi nyumbani nikijilaumu kufanya kitendo hiki lakini nkajiambia Si ATANIOA!!!

Zikapita Takribani siku 3 kimya kijana apigi simu mara wakakutana njiani Binti akamwambia mbona kimya hapana usijali basi panda kwenye Gari twende wapi Binti akauliza ? Akajibu kijana kwenye ile Nyumba Yetu binti akakataa jamaa akatoa Cd akamwambia humu kuna kila kitu tulichokifanya siku ile usipopanda kwenye Gari naisambaza Cd hii Binti wawatu kwa kuogopa usianikwe uovu alioufanya akabidi apande Gari ...!

Binti anasema nikawa kama mtumwa wa ngono kwake ananichukua na kwenda kunizini kisha jamaa baada ya kumchoka Akampa Ndugu mmoja wa Binti ile Cd akampelekee Baba mzazi wa Binti alivyoiangalia Cd hiyo Mzee wa watu akapandisha Pressure akapelekwa Hospitalini na akifia huko!!!!

Baada ya Msiba wa Mzee kutokea Mama mtu naye kwa machungu mazito yakuondokewa na Mume akapata Mshtuko nae akafariki Dunia Binti akawasabishia uyatima ndugu zake wadogo.

Binti kwa hasira na uchungu wa kupoteza wazazi wawili akaamua kuchukua Kisu na akampigia simu yule jamaa wakutane kwenye ile Nyumba Baada ya kuingia nae chumbani Binti kwa Ghafla akatoa kisu na kumchoma yule kijana kijana akainamia chini na Kufariki!!!

Baada ya kufanya tukio hilo Binti anasema akajisalimisha kituo cha polisi na Ana subiri hukmu yake

Kisha akasema natamani wasichana wote wasome mkasa huu ili wajue jinsi gani wanaume walivyokuwa waovu kama Mbwa Mwitu kisha akasema mabinti msikubali kudanganywa mkajakujuta Majuto Makubwa.....!!!!


Nawasilisha.........!!!!
 
Hizi hadithi zisizo na uhalisia peleka chukwa la wavuta unga... Sasa wewe unakufaje kwa presha kwa kuwa tu binti yako kaliwa mzigo. Ulipomwona amezaliwa na kitundu unadhani kilikuwa cha matumizi gani? Huyu mzazi naye ni mjinga...
True story
 
Huyo mzee alikuwa na roho nyepesi,,alitakiwa amsifie binti yake na amshauri afurahie ila asiwe anajirekodi.
 
Wajameeeni duuuu hata km ni mm mmmhh.........!!!!!!!!.......(.....)
 
Mmmhhh Tafadhali sana..! Sisi ni mbwa mwitu tena...! Hawa wanawake Hawa yaani na kuwapa mbavu moja bado wanatutusi.? Najiuliza kama mbwa mwitu alitolewa mbavu moja na ukawekewa ukaitwa Hawa..? Wewe ni nani
Nia yake haikuwa mbaya nadhani ni kutokana na ukatili aliofanyiwa na huyo bwana Uchwara!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom