Kwanini wengi hupenda kujihukumu?

Kwanini wengi hupenda kujihukumu?

MwakiIV

Member
Joined
Aug 31, 2018
Posts
79
Reaction score
142
Tafiti zinasema wanadamu wengi hukata tamaa baada ya swali hili “Kama hatuwezi kushinda kwa nini tushindane?”

Watu wengi hawashiriki michakato ya ushindani kama watahisi kuwa kuna dalili ya aidha upendeleo au pengine mtu ujipima kwa sifa zilizolengwa.

Wengine huacha kuendelea kuomba fursa ya kazi/biashara kwa sababu ya washindani wenzie kitu ambacho si sahihi sana.

Kwa ujihukumu?
Kazi yako ni kushiriki na kazi ya kuhukumu ni ya wengine, mbona usifanye upande wako na upande mwingine umwachie mwingine na Mungu wako?

Kughairi kwa kila jambo ni kujifungia milango ya fursa, kuna watu wengi hawajui vitu vingi na wapo sehemu wanafanya vitu ambavyo pengine ungeweza kufanya kwa ufanisi zaidi. Lakini hutaki kuonesha unajua au hutaki kuomba.

ANZA SASA omba fursa unayotamani, nenda unapoona kuna fursa, mawazo yako yasikurudishe nyuma, hakuna kitu tofauti sana kisichoelezeka na kueleweka.
 
Back
Top Bottom