Kwanini waziri wa viwanda na biashara asiachie ngazi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwa nchi za wenzetu kama kuna mtikisiko wa kiuchumi taifa zima kwa kusababishwa na kuyumba kwa bidhaa flani basi waziri husika huwajibika haraka ili kuonesha uwajibikaji kua ameshindwa kwa nguvu zake zote na kiashiria kua hali sio nzuri.Wengi wanaweza kunitupia mawe juu ya hili lakini ukweli ndio huo.

Hili tatizo halimhusu sana waziri wa kilimo na chakula na uvuvi japo ni mtambuka lakini kwa kiasi kikubwa ni wizara ya biashara na viwanda. Ni kwanini waziri huyu hakuchukua jitihada za ziada kumweleza rais hali halisi ilivyo baada ya kufikia maamuzi ya kuzuia uingizwaji kutoka nje! Sukari haijawahi kushuka bei tangu Mh Rais atangaze kuzuia uingizwaji wake kutoka nje, sukari haijawahi kushuka bei tangu bodi itangaze bei elekezi.

Kama kweli tatizo lilikua linafahamika tangu awali kulikua na upungufu mkubwa wa sukari nchini kwanini waziri pamoja na wataalamu wengine wa wizara wasingekaa na Mh Rais wakamweleza hali ilivyo? Au walikua hawajui kua kuna tatizo tayari? Hapa bila kupepesa macho kuna uzembe ulifanyika tangu swali.

Kuna fununu kua baadhi ya viwanda vya uzalishaji wa sukari nchini viko katika hali ya matengenezo! Swali je, kwanini wizara hawakutahadharisha mapema kutokana na tathmini ya kiwango cha sukari kilichokuwepo nchini? Inakuwaje viwanda vinakua katika hali ya matengenezo muda ambao upatikanaji wa sukari ulikua hauridhishiji? Je, takwimu wanazotumia zina ukweli wowote?

Kwanini mpaka leo waziri hajavunja bodi ya sukari kwa kushindwa kazi?

JE, WAZIRI ANA MAKOSA?
Hata kama pengine tatizo ni natural kulikua na uwezo wa kuzuilika lakini limemkuta ndani ya wizara yake ni lazima awajibike! Kwa nchi za wenzetu huyu waziri angeshajiuzulu siku nyingi!

Waziri anaweza kulalamika kua yeye hahusiki lakini huo ndio unaitwa uwajibikaji wa kisiasa. Ni bahati mbaya kwake, ajali inemkuta mikononi mwake hakuna namna.
 
Haijalishi atajitumbua au laah! Kinachotakiwa ni uwajibikaji.
Ndugu yangu unategemea ufanisi gani toka kwa mawaziri ambao kila wakisimama kusema kauli zao ni "The Rais aliagiza, Rais wetu anataka hivi, Nampongeza sana Rais kwa kuagiza vile, serikali ya the Magu inasisitiza kuwa, nk Nk" ??
Hawa wote ingekuwa kama Kule mfumo wa kuwa under probation kwa miezi 6 unatumika (ajira zingine) nadhani baada ya hii 6 kupita kama kuna mawaziri wakubaki kazini wasingezidi 30%
 
Ofisi ya waziri mkuu Awamu hii ya magu ana wizara ngapi chini yake?
 
Huyu jamaa tatizo ni muongeaji sana ila vitendo ni zero, yeye ni kuongeaga maneno matamu tu!
 
Cheo cha zawadi atajiuzulu vipi mkuu.
 
Huyu jamaa tatizo ni muongeaji sana ila vitendo ni zero, yeye ni kuongeaga maneno matamu tu!
Hili tatizo la sukari linamhusu sana! Watu waongeje sana si wa kupewa nafasi za juu hata kidogo. Mtu anakua muongeaji lakini kazi hakuna maana yake nini.
 
Ndugu yangu unategemea ufanisi gani toka kwa mawaziri ambao kila wakisimama kusema kauli zao ni "The Rais aliagiza, Rais wetu anataka hivi, Nampongeza sana Rais kwa kuagiza vile, serikali ya the Magu inasisitiza kuwa, nk Nk" ??
Hawa wote ingekuwa kama Kule mfumo wa kuwa under probation kwa miezi 6 unatumika (ajira zingine) nadhani baada ya hii 6 kupita kama kuna mawaziri wakubaki kazini wasingezidi 30%
Huu mfumo sijui utakuja kufia kwenye mikono ya nani maskini.
 
Back
Top Bottom