Kwanini watu wanene/Vibonge wanahisi njaa mara nyingi na hupenda kula kula sana?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,585
15,366
Dubu ni mnyama ambaye ukikaribia wakati wa baridi Kali, hula Chakula na kunenepa na anaweza kukaa hata mwezi bila kula wakati huo akitumia Akiba za Mafuta mwilini mwake.

Nashangaa vibonge wengi nilitegemea wawe wazembe kwenye kula. Ikiwezekana wapitishe hata siku mbili kavu bila kutetereka.

Mfano unakuta mtu anakilo 100. Ktk hizo Lita kama 5o ni Mafuta. Mafuta hayo ni Chakula cha Akiba lkn wengi ni walafi, wananjaa muda mwingi, wanakula mno tena vitu wasivyotakiwa kula.

Mfano
Kuna Bonge mmoja ukimpa kilo tano za kitimoto dakika 10 anafuta.

Kuna wazungu mabonge niliwaona mbuzi mzima anaweza kufutwa na watu watatu tu.

Je, Tatizo ni nini? Sensa za misosi huwa zinakata?
 
Kupenda kula kula Ni addiction Kama addictions nyingine tu, Ni sawa na mtu ambaye hawezi pitisha siku bila kunywa Pepsi bariiiiidii na asipokunywa siku hiyo haijapita!! Lakini tunajua kabisa Pepsi SIO kilevi nadhani Ni suala la kisaikolojia Leo mtu huyo huyo akiamua kubadilisha lifestyle yake baada ya wiki tu atazoea na hatokuwa anahisi njaa mara kwa mara Kama ilivyokuwa hapo awali kwasababu Ni suala la kisaikolojia tu.
 
Sio kwamba wanakuwa na njaa kila muda... Nikupenda kula kula hovyo...

Mtu kila muda unakuwa unakula tu
 
kinachomfanya mtu kuwa kibonge ni ka vitu viwili tuu, yani CHAKULA na Kurithi vina saba.
 
Back
Top Bottom