The Humble Dreamer
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 7,442
- 10,233
Wakuu Salaam,
Nimeamkia bucha moja huku niliko nipate nyama nitengeneze mtori, sasa hili bucha linalofungua mapema liko karibu na Kanisa na linauza sana maana watu wakitoka tu ibadani wanajazana pale.
Nilichoshangaaa watu walioko ibadani hawajavaa Barakoa..yani kuanzia muhubiri, waongoza nyimbo, kwaya, watumishi wote mle ndani hawajavaa.
Hili nimelijua kwa njia 3
Moja, bucha lilipo si mbali na kanisa, na mtu akivaa barakoa inaonekana kwa ungaaji wake mana nyingi rangi zina mng'ao. Najua ziko nyeusi pia. Hata mwitikio wa sauti za nyimbo au kujibu 'Amen' ungekua wa chini kama wamevaa barakoa. Lakini wanashangilia kabsa.
Mbili, ni kwamba Nimemuuliza muuza nyama, vipi Ibada ya kwanza watu walikua wamevaa Barakoa? Amejibu 'watu wakiwa ibadani hawavai lakini wakishatoka tu huko Ibadani ndiyo wanaanzia kuvalia hapa buchani kwangu na wengine hawana kabsa.'
Tatu, njia inayoelekea nakokaa nako kuna kanisa, na muda huu asubuhi ndiyo nyimbo za kusifu. Sasa watu wamejiachia wanacheza tu. Hili kanisa halijamaliziwa madirisha yake kwahyo unawaona moja kwa moja. Siyo muhubiri siyo muumini au waimbishaji wote hawajavaa Mask.
Na hii hali inaonekana ni kwa Ibada nyingi hapa Tz.
Watu hao hao wa Ibadani unakutana nao stendi wamevaa, sokoni wamevaa, kwenye gari wamevaa, benki wamevaa nk. Lakini Ibadani hawavai.
Huu ujasiri wa kutovaa barakoa wanautoa wapi?
Hii hali inatia huzuni maana hakuna anayejua afya ya mwenzake hasa ukizingatia hiki kirusi kinaeza kutulia tu ndani ya mtu huku kikiendelea kukutengeneza taratibu na huku ukiendelea kuambukiza wengine. Saa kikichanganya ni kimeamka kweli.
Watu wanatakiwa kuchukua hatua kwa mazingira yote.
Stay Safe.