Wengi wao utakuta wanaongea kwa sauti ya juu sana kuliko kawaida, anakuongelesha kwa sauti ya juu kana kwamba uko mita 25 toka alipo; nini tatizo au chanzo chake?
Kuna mzee mmoja hakuwa kicheche lakini mke wake alikuwa mgawaji hatari, mke alikufa kwa ukimwi, na mzee aliambukizwa na mkewe. Sasa kipindi nimepanga kwake, alikuwa ni mtu wa kufokea watoto kwa sauti ya juu sana, na ilikuwa kila siku, hata kama hawajakosea, na hata akiwa anawatuma vitu, au anawaita, hata wakiwa karibu ilikuwa ni kwa sauti ya juu. Yeye ndiye alinisimulia kuwa kaambukizwa virusi na mkewe, lakini maisha ya kabla mkewe hajafariki siyajui (yaani kama alikuwa anapayuka au la). Ningekuwa nilimuona kabla mkewe hajafariki kwa ngoma, ningesema hiyo ni kweli au la. Naishia hapo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.