Fernando Wolle
JF-Expert Member
- Aug 19, 2022
- 387
- 775
Kwanza naamini hakuna Mtanzania ambaye hajui umuhimu wa kulipa kodi, kila mwananchi anatambua umuhimu wa kodi. Na hakuna serikali duniani inayoweza kuendeshwa pasipo kukusanya kodi.
๐๐ธ๐ข๐ฏ๐ช๐ฏ๐ช ๐ธ๐ข๐ฏ๐ข๐ฏ๐ค๐ฉ๐ช ๐ธ๐ฆ๐ฏ๐จ๐ช ๐ธ๐ข๐ฏ๐ข๐ญ๐ข๐ญ๐ข๐ฎ๐ช๐ฌ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฉ๐ถ๐ด๐ถ ๐ต๐ฐ๐ป๐ฐ?
Licha ya tozo hizi zinazolalamikiwa hapa kutokuwa na ufafanuzi wa kutosha wala kutolewa Elimu ya kutosha kutoka kwa wanaotoza kwenda kwa wanaotozwa, bado zinaonekana zina mapungufu na kuna maswali mengi kuliko majibu.
๐๐ฐ๐ป๐ฐ ๐ป๐ช๐ฏ๐ข๐ป๐ฐ๐ญ๐ข๐ญ๐ข๐ฎ๐ช๐ฌ๐ช๐ธ๐ข ๐ฉ๐ข๐ฑ๐ข ๐ฏ๐ช
1. ๐๐ฐ๐ป๐ฐ ๐ป๐ข ๐ฎ๐ช๐ข๐ฎ๐ข๐ญ๐ข ๐บ๐ข ๐ด๐ช๐ฎ๐ถ
2. ๐๐ฐ๐ป๐ฐ ๐ป๐ข ๐ฎ๐ช๐ข๐ฎ๐ข๐ญ๐ข ๐บ๐ข ๐ฃ๐ฆ๐ฏ๐ฌ๐ช
3. ๐๐ฐ๐ป๐ฐ ๐ป๐ข ๐ท๐ช๐ฏ๐จ'๐ข๐ฎ๐ถ๐ป๐ช
Kwa ujumla ni tozo zote za Kielekroniki.
Katika hali ya kawaida ni kwamba tozo hizi zinaonekana kukatwa mara mbilimbili pasina kuwa na sababu maalum.
Mathalani, mfanyakazi/Mtumishi anayelipwa mshahara hukatwa Kodi na Serikali kwenye PAYE, pia kuna Makato mengine kama ya NSSF/PSSSF, Bima na mengine yanayofanana na hayo. Makato haya hufanyika kisha mshahara wa mfanyakazi (take home) huingizwa kwenye akaunti yake ya benki husika.
๐ด๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐! Mshahara huohuo ambao umeshakatwakatwa, mfanyakazi anapokwenda kuchukua haki yake anakutana na Serikali iko pale inasubiri tena kwa mara ya pili kitu kinaitwa tozo, Sasa hapa serikali inakuwa imewekeza nini? Kwasababu kwa mara hii Makato yalipaswa kuwa ya benki Pekee (๐ด๐ฆ๐ณ๐ท๐ช๐ค๐ฆ ๐ฑ๐ณ๐ฐ๐ท๐ช๐ฅ๐ฆ๐ณ) ambapo mteja hukatwa kulipia gharama za huduma ila hapa tuulize kiungwana kabisa Serikali yenyewe inakuwa imefanya nini mpaka kukata mara ya pili?
Mfano mwingine, mfanyabiashara analipa Kodi ya serikali moja kwa moja kwa TRA, anapambana kupata faida kidogo anaweka benki, akihitaji kuchukua pesa yake benki anaikuta Serikali tena kwa mara ya pili inasubiri tozo. Huku ni kulipishwa Kodi mara mbilimbili isipokuwa Majina ya Kodi ndio yanatofautiana. Sasa huu utitiri wa tozo una tofauti gani na Kodi za kipindi cha ukoloni? Mfano poll tax, hut tax, matiti tax, n.k.
Tukienda kwenye tozo za miamala ya simu ni kitu kilekile na tukirudi kwenye tozo za king'amuzi mambo ni yale yale ya serikali kuvuna mahali ambapo haijapanda, ili serikali isilaumiwe iende na kanuni ya kuwekeza na kuvuna na sio kuvuna bila kuwekeza tofauti na hapo ni kuua uchumi wa watu na ๐ง๐ช๐ฏ๐ข๐ญ๐ญ๐บ taifa litayumba kiuchumi.
๐๐๐๐๐๐๐๐๐: Miaka mitano iliyopita serikali ilibuni vitambulisho vya Wamachinga japo kuna watu walipinga lakini ule angalau ulikuwa ni ubunifu wa kukusanya mapato ya serikali ambao tunaweza kusema ulikuwa ni '๐๐ถ๐ต๐ถ๐ข๐ญ ๐ฃ๐ฆ๐ฏ๐ฆ๐ง๐ช๐ค๐ช๐ข๐ญ' . Ilikuwa Machinga akilipia elfu ishirini anaona kuna sababu kwanini amelipia. Anaruhusiwa kufanya biashara kwenye miundombinu ya serikali, hiyo ni sababu tosha kabisa kwamba serikali inakuwa imefanya kitu kwa huyu mtu anayetozwa hiyo kodi.
Uwekaji wa tozo hizi za sasa unaashiria ubunifu hafifu wa ukusanyaji mapato. Tanzania kama nchi tumebahatika sana kuwa na rasilimali nyingi zinazoweza kuingiza mapato makubwa kama kutakuwa na usimamizi madhubuti.
Rai ni kwamba viongozi wanaohusika na mikakati ya ukusanyaji mapato, wapende kuumiza vichwa kupata njia bora ya kukusanya mapato na sio kutumia njia rahisi namna hii.