kipanga mlakuku
Member
- Jun 9, 2011
- 92
- 53
Umofia Kwenu, Wadau nimetembelea vituo kadhaa vya kujiandikisha naona hamasa imekuwa kubwa, hivi kwanini? watu wanataka mabadiliko? kweli watapiga kura? au wanataka vitambulisho kwa ajili ya kufungua account bank? nashindwa kuelewa, nahisi kama lilikuwa chezo ili watu wasijitokeze ili wahafidhina wa CCM ndo wajiindikishe, lakini upepo umebadilika, kila mv kadhamiria
Mkuu, haha watu wa makerting wanasema ukiona wateja wamekosa hamasa na bidhaa yako basi unatakiwa ufanye STIMULATION AND CONVENTION MARKETING na njia mojawapo ni kubadilisha product features, sasa mkuu hivi vikadi vya sasa ni vizuri(wamebadili features) kuliko vile vya zamani , vijana wa "kwetu" wamevipachika jina viATM. watu wanataka hivyo vikadi na wala sio kupiga kura!
Aione: Mkoroshokigoli
Umofia Kwenu, Wadau nimetembelea vituo kadhaa vya kujiandikisha naona hamasa imekuwa kubwa, hivi kwanini? watu wanataka mabadiliko? kweli watapiga kura? au wanataka vitambulisho kwa ajili ya kufungua account bank? nashindwa kuelewa.
Nahisi kama lilikuwa chezo ili watu wasijitokeze ili wahafidhina wa CCM ndo wajiindikishe, lakini upepo umebadilika, kila mtu kadhamiria
Watu walivyoichoka CCM,Wamedhamiria kuichinjia Baharini kimyakimya.
Upo sahihi kabisa mdau,watu wanahitaji kadi na si kwa ajili ya kupiga kura.Kwa usumbufu wanaoupata kwenye kujiandikisha naamini watarudia ya 2010 hawatapiga kura,kwa sababu zoez zima la uandikishaji ni adhabu hata maombi ya VISA ya kwendA USA hayawi vile.Watu wanataka kadi kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku kama nyaraka muhimu itakiwayo na mamlaka au taasisi mbalimbali.
Sidhani kama nia yao ni kitambulisho watu wanataka mabadiliko tena wakati uu vijana ni wengi sana. Watu siku hizi wamebadilika sana tofauti na zamaniWatu wanataka vitambulisho ndio maana wako radhi kuvumilia adha zote wakati wa kujiandikisha. Sasa subiri kimbembe siku ya uchaguzi amini nakwambia siku hiyo kama kutakuwa hivi hivi watakao piga kura ni aslimia 25% tu