Unazungumzia mafanikio gani ? ya umaarufu au ya kiuchumi ?.....na hiyo "nje" unayoizungumzia ni Ulaya, America, Asia au sehemu nyingine ya Africa ?
Hata mafanikio ya wanamuziki wa kiafrika nje ya nchi zao ni mmoja mmoja sana, na huwezi kulinganisha na wanaofanyia shughuli zao Marekani....unachokifanya Marekani ni rahisi kuonekana duniani kutokana na ukubwa wa Marekani....hata Ulaya, Asia na America kusini nao wanatoka mmoja mmoja sana na mara nyingi wanalazimika kuhamia Marekani kwa mafanikio zaidi.
Kwa kuwa tu unaangalia muvi za Hollywood haimaanishi dunia iliyobaki imeacha kutengeneza filamu la hasha, ukweli ni kwamba Ulaya na Asia wapo mbali sana na wanazalisha filamu kila kukicha na zinakidhi masoko yao...ila linapokuja suala la kidunia, Hollywood ni level nyingine.
Sasa je, unawalinganisha wasanii wetu na wale wa Marekani na ulaya ? na kama ni mafanikio ya kikazi kibongobongo mbona tulishakuwa na akina Marehemu Marijani, Remmy, Ngurumo n.k ingawa kiuchumi ndio hawakufanikiwa.