Kwanini viongozi wa vyama vya upinzani hawabadiliki?!

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
453
635
Miaka nenda miaka rudi, viongozi wa labda CHADEMA, CUF, TLP nakadhalika ni WALEWALE TU?! Kwanini hawateuliwi au kuchaguliwa wapya kama CCM? Je wanachama wa hivi vyama hawana upeo au "options" ya kuchaguwa viongozi wapya bila kujali dini, kabila umri au elimu na wenye mawazo mapya?
 
Viongozi wa upinzani unataka wabadilike ili iweje............

Sasa kwa taarifa yako shida ya watanzania tunataka maisha bora,elimu bora, chakula bora hebu timizeni ahadi mliozotuahidi
 
Miaka nenda miaka rudi, viongozi wa labda CHADEMA, CUF, TLP nakadhalika ni WALEWALE TU?! Kwanini hawateuliwi au kuchaguliwa wapya kama CCM? Je wanachama wa hivyi vyama hawana upeo au "options" ya kuchaguwa viongozi wapya bila kujali dini, kabila umri au elimu na wenye mawazo mapya?!

Naamini kila chama kina miongozo yake, na kutokana na hiyo miongozo huendesha chaguzi mbalimbali kila baada ya muda fulani. Kwa wao kubadilisha viongozi ama kuto badilisha inategemea na miongozo hiyo sambamba na matakwa ya wapiga kura wao (WANACHAMA).

Kwamtazamo wangu sioni kwanini ushughuliswe na viongozi wa vyama ambavyo wewe si mwanachama, na kwa vyovyote hufahamu malengo ya hivyo vyama wala malengo na mitazamo ya wanachama wake.

Hivyo nakushauri Uhangaike zaidi na chama chako kinafanya nini katika kutimiza malengo yake na si CHAMA CHA JIRANI HAKIFANYI NINI?
 
mbona chadema wanafanyaga uchaguzi wa ushindani
ccm mwenyekiti anashindanishwa na kivuli
 
Viongozi ambao hadi sasa wanaonyesha ueleko wa viongozi wa maisha ni

1.MWENYEKITI MPENDWA KIONGOZI WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CHADEMA MHESHIMIWA KIM JONG UN MBOWE WA CHADEMA

2.MFALME KYABAZINGA KABAKA MREMA WA TLP

3.MFALME AKIHITO CHEYO WA UDP

4.AYATOLAH SEIF SHARIF HAMAD WA CUF

5.MFALME MSWATI MBATIA WA NCCR

6.CHIFU FAHMI DOVUTWA WA UPDP
mambo mengine yabidi mtu ucheke tuu hata km inauma
 
Viongozi ambao hadi sasa wanaonyesha ueleko wa viongozi wa maisha ni

1.MWENYEKITI MPENDWA KIONGOZI WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CHADEMA MHESHIMIWA KIM JONG UN MBOWE WA CHADEMA

2.MFALME KYABAZINGA KABAKA MREMA WA TLP

3.MFALME AKIHITO CHEYO WA UDP

4.AYATOLAH SEIF SHARIF HAMAD WA CUF

5.MFALME MSWATI MBATIA WA NCCR

6.CHIFU FAHMI DOVUTWA WA UPDP
Ili usiwe kiongozi wa maisha kwa mujibu wa wewe basi inabidi Uwe unachaguliwa kila baada ya Miaka 10 kama wanavyofanya CCM ambao ndio Rais wa Nchi amekua akitokea huko. Bahati mbaya hii kwako ndio umeichukulia kama "Marking Scheme" ambayo unataka kila chama kiifuate ili kisionekane kua kina Mwenyekiti wa Maisha.

Bahati mbaya sana akili zako za kilumumba ambazo ule ukijani umezifunga zikashindwa kunyambua hili swala zinashindwa kukwambia Sio lazima kila Chama kiwe na Utaratibu ule ule sawa na wa CCM na ndio maana vikaanzishwa vyama vya upinzani ili kila chama kilete sera tofauti. Ingekua Vyama vya Upinzani vinakubaliana kila kitu na CCM basi hakungekua na haja ya vyenyewe kuwepo sababu vile ambavyi vinapiganiwa ndio vinavyofanywa na CCM

Akili zako za Kilumumba pia zinakuzuia kuwaza kua kwa kua Katiba ya Nchi inalazimu Rais kukaa Miaka isiyozidi 10, basi nanyi CCM mnalazimika kutomuweka Mwenyekiti wenu zaidi ya hiyo Miaka 10 ili muda mwingi Rais wa Nchi ndio awe Mwenyekiti wenu. Utaratibu huu wewe akili yako ya Kilumumba inataka uwepo mpaka kwenye Vyama vya Upinzani ilhali havijatoa Rais wa Nchi.

Akili yako inashindwa kukumbuka kua Hayati Baba wa Taifa alikaa kwenye Uongozi wa Chama kwa Miaka Mingi tu sababu hata Urais aliokua akiushikilia ulikua pia ni wake miaka yote hiyo aliosimamia Chama. Siwezi kukulaumu sana kwa kutojua hili maana hauko peke yako hapo Lumumba hivyo kwa kua kila unaemuangalia hapo basi unamuona mnafanana akili, hamtoweza kuwaza nje ya hapo.

Tumia Kichwa kufikiri, na sio kufugia Nywele.
RIP Dkt Didas Masaburi
 
mbowe alishindana na nani
FREEMAN MBOWE ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA
Jamii
Posted On Monday, 15 September 2014 04:15 Written by mjengwablog
Rate this item
(0 votes)
CHADEMA2.jpg


Freeman Mbowe akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.

Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa baada ya kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani wake Ngambaranyela Mongatero akipata kura 20.

CHADEMANEW.jpg


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.

Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.

Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163.GPL(P.T)
 
Siasa za bongo ni usanii mtupu,,,acha nihangaike na maisha,,, ingawa huyu msukuma anawamaind mno wageni/wawekezaji na ndio wametuajiri na sio serikali,,,bila ya wao tusingefyatua watoto....


I miss you JK,,,weye ni jembe hakuna akufikiae.
 
By Prof: Balegu wa chadema

Vijana ndo wajinga sikuhizi sio wazee. Chadema chama cha vijana wapenda mabadilikoo. Mbowe Kim Jong Un. mfalme.
 
Mada ya kipuuz kabisa

Ova
Duniani hakuna kitu cha kipuuzi, kilichopo ni tofauti za mitazamo tu. Kile kitu ambacho kwako ni haramu kwa mwingine ni kivuno. Tujifunze kuzikubali na kuishi nazo kwa amani hizi tofauti zetu.
 
Back
Top Bottom