Kwanini vijana wa sasa hawadumu kwenye mahusiano kama babu zetu?

SIREN

Member
Sep 5, 2013
77
44
Habarini wana Jamvi,

Natumaini mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na kazi zenu za kila siku.

Napenda kuleta kwenu mjadala huu;

Hivi ni kwanini vijana wa sasa walio wengi hawadumu kwenye mahusiano tofauti na mababu zetu ambao hawakuwa huru kujichagulia wanaowapenda?
 
Umegonga penyewe kabisa Mkuu technology imechangia sana kuvuruga mahusiano Tanzania sijui kama kuna tatizo kama hili nchi nyingine.

Kuna watu wa jinsia zote kutwa kucha ni kuwaponda wanaume na wanawake utadhani hakuna wanaume na wanawake wenye sifa chungu nzima za kuwa waume/wake bora ndani ya ndoa.

Hata hapa JF hili linaanza kuota mizizi. Mie linanikera sana kusema kweli ila sijui nini cha kufanya ili kupambana nalo hili.

Tatizo utandawazi umezidi, enzi za mababu hakunaga mambo hayo
 
una ushahidi wa uyasemayo?
Ndio, kila mtu ushahidi anao tena wa kutosha. Miaka ya m ababu zetu ilikuwa kawaida kabisa kumkuta kijana wa miaka 25 akiwa hajawahi kusex kabisa, lakini kwasasa ni nadra sana kumkuta kijana wa miaka 15 akiwa hajawah kusex. Masuala ya talaka, mimba za utotoni na magonjwa ya zinaa siku hizi ndo fashion jambo ambalo enzi hizo ilikuwa ni mambo ya aibu kabisa kwenye jamii.
 
1. Tunaongozwa na tamaa... Mababu zetu walikua wanaingia kwenye mahusiano kwa lengo la ndoa, na wanaweza kaa miaka bila sex wakisubiri ndoa. Sasa hivi wengi wanaingia kwenye uhusiano kwaajili ya sex.
2. Hamna mda wa kumfahamu mtu kabla haujatongoza au kukubali mtongozo. Ule utamaduni wa kumchunguza mtu kabla ya kuanzisha uhusiano haupo kwa wengi wetu. Mtu mnatingozana JF mnakutana siku ya kwanza na sex juu eti ndo uhusiano ushaanza hivyo...
3. Wengi tunaingia kwenye mahusiano bila kujifahamu sisi wenyewe vizuri na kujua mtu wa namna gani anatufaa. Ko tunajikuta kila uhusiano tunaoingia tunakuta kasoro nyingi tu.
4. Tamaa zimezidi sana
 
Unadhani nini kifanyike?
 
Back
Top Bottom