Kwanini upinzani umekubalika Mikoa ya Mara na Mbeya ukilinganisha na Mikoa mingine?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Baada ya kuzunguka na kutembea mikoa karibia 20 hapa tanzania kuna utafiti nimeufanya kuwa siasa za upinzani kwa muda mrefu zimekubalika sana haswa mkoa Mara na mbeya.

Upinzani uliopo katika mikoa hii miwili haupo tuu mjini lakini hadi vijijini upinzani umeweza tofauti na mikoa kama Kigoma, Iringa,Arusha,Morogoro,Singida, Kilimanjaro,Dar na kwingineko upinzani ambapo upinzani huwa ni huja kwa msimuu.

Mikoa ya Mara na Mbeya upinzani ulianzia tangu NCCR Mageuzi 1995 upinzani umekuwa mkubwa kiasi kikubwa na hadi sasa chama kilichoshika hatamu ni CHADEMA,

Licha ya maneno mengi na propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa Kaskazini lakini huku Mara na Mbeya watu wamekikubali japokuwa mwasisi wa CCM alitokea mkoani Mara lakini huku Mara bado upinzani una nafasi sana.

Swali langu. Je, ni kweli watu wa Mara na Mara wanaojitambua kuliko wengine au watu wa maeneo ya huku wanajitambua au wamepotea?

Je, ni kwanini watu wa Mara na Mbeya wanapenda sana upinzani?
 
Kuna harufu ya ukweli kiasi...

Mkoa wa Mara 2015 upinzani awakuwa makini tu wangechukua majimbo yote isipo kuwa jimbo la mwibara kwa kangi.

Walizubaa wakapigwa za uso jioni badala ya asubuhi...
 
Kuna harufu ya ukweli kiasi...

Mkoa wa Mara 2015 upinzani awakuwa makini tu wangechukua majimbo yote isipo kuwa jimbo la mwibara kwa kangi.
mkuu wakati nipo mkoani mara kuna jamaa aliniambia mkoa wa mara hawanaga desturi ya kumpa mwanamke uongozi katika maswala ya siasa.

lakini safali hii unambiwa mwanadada easter bulaya wa bunda na mwanadada easter matiku kupitia chadema waliweza kushinda katika majimbo yao na kuwagalagaza wanaume
 
Wana Mara Tunaichukia CCM kwa sababu mwasisi wake hakuwa tiyari kuwaletea wana mara maendeleo,mfano ziwa viktoria lipo karibu,ila maji majumbani hamna.ila nenda mikoa mingine maji hadi chooni.hakika hatuipendi ccm.
 
Mkoa wa Mara wanapakana na nchi ya Kenya na Mkoa wa Mbeya wamepakana na Zambia nchi ambazo raia wake wamekataa
Kutumikishwa na chama kimoja.
 
Nakumbuka stori ya mwalimu Nyerere alipotishia kumpigia kura mgombea wa upinzani, mara baada ya kugundua kuna figisu CCM zinachezwa ndani ya chama kuhakikisha mgombea wa Ubunge Musoma anayekubalika anapigwa chini.

Mara ni habari nyingine aiseeee, UKAWA walicheza mistake sana mwishoni majimbo yote wangebeba kasoro kajimbo kamoja tu.
 
Kwasababu Mikoa Ya Mara, Kilimanjaro, Mbeya Na Arusha Ndio Mikoa Inayoongoza Kwa Kuwa Na Vijana Wengi Wala Bange Aka Ndumu. Na Kama Ujuavyo Wala Ndumu Huwa Wanajifanya Wanaharakati Sana
 
Kwasababu Mikoa Ya Mara, Kilimanjaro, Mbeya Na Arusha Ndio Mikoa Inayoongoza Kwa Kuwa Na Vijana Wengi Wala Bange Aka Ndumu. Na Kama Ujuavyo Wala Ndumu Huwa Wanajifanya Wanaharakati Sana
Ha ha ha kweli wewe ni kiazi kilichochipua kipindi cha ukame.

Wala bange wanafanya maamuzi sahihi kuliko wewe mnywa viroba vya mia tano.
 
Back
Top Bottom