Kwanini Uovu (Evil) ni Asili – Why Evil is Natural

Spinozist

Senior Member
Joined
Feb 26, 2025
Posts
120
Reaction score
158
Kwanza, Ni nini maana ya Uovu/Ubaya? Katika mantiki ya Sheria za Kiasili, Uovu si nguvu ya kiroho inayojitegemea, bali ni tafsiri ya kibinadamu juu ya matokeo ya michakato ya kiasili inayosababisha Maumivu kwa Kiumbe Hai chenye uwezo wa kuhisi. Viumbe hai wengi wana mfumo wa neva wenye nociceptors (pain receptors), Hizi si za kimaadili bali ni za kibayolojia, na kazi yake kuu ni Survival.

Mfano: Binadamu akiweka mkono wake kwenye Moto, maumivu hutokea. Moto haukusudii kuumiza, joto linafuata sheria za fizikia. Maumivu ni signal ya mwili kujilinda dhidi ya uharibifu wa tishu. Swali ni kwanini kuna pain receptors? Jibu ni kwamba bila maumivu, kiumbe hai angeweza kujiua bila kujua. Maumivu ni mfumo wa tahadhari wa kiasili. Kwa mtazamo wa Charles Darwin, miundo ya viumbe hai haikutengenezwa kwa misingi ya maadili bali kwa ajili ya kuendelea kuishi kupitia natural selection.
Hivyo Maumivu ni Asili, na kile tunachokiita Uovu ni tafsiri yetu juu ya maumivu hayo.

Je, Dunia ingeweza kuwapo bila Maumivu?

Ndiyo, ingeweza kuwapo kama mfumo wake ungekuwa tofauti. Lakini Dunia iliyopo sasa inaendeshwa na Sheria za Kiasili ambazo hazina nia wala maadili.

Mfano, Tetemeko la ardhi: kwa macho ya kibinadamu ni janga na ni uovu mkubwa, lakini kwa jicho la kiasili ni matokeo ya plate tectonics. Dunia haichagui kuua, inafuata sheria zake. Miili inayokufa inaingia kwenye mzunguko wa kibaolojia: kuoza, kuwa virutubisho, kuwa sehemu ya mfumo mwingine wa uhai. Hapa hakuna nia, hakuna chuki, hakuna hukumu ya maadili. Asili si njema wala si mbaya, ni mfumo unaojiendesha kama alivyosisitiza Baruch Spinoza.

Pili, Uovu na Dhambi. Ili Uovu kuwapo hauhitaji imani juu ya Mungu. Maumivu yalikuwepo kabla ya dhana ya Dhambi. Lakini Dhambi haiwezi kuwapo bila Mungu, kwa sababu Dhambi ni kuvunja amri ya Mungu. Hivyo Uovu ni matokeo ya michakato ya kiasili yanayosababisha maumivu, wakati Dhambi ni dhana inayotegemea uwepo wa Mungu.

Ikiwa Mungu anachukizwa na Binadamu kumuua Binadamu mwingine, kwanini hachukizwi na Binadamu kumuua Mnyama kwa ajili ya chakula? Kwanini hachukizwi na Simba kumuua Swala kwa ajili ya chakula?

Kama jibu ni kwamba wanyama hawana moral agency, basi maadili yanamhusu nani? Kama maadili yanamhusu tu Binadamu, je mateso ya viumbe wengine hayana uzito wa kimaadili? Pia Je, ni nini hasa kinachofanya kitu kiwe na uzito wa kimaadili?

Kama Mungu ndiye muamuzi wa mwisho wa lipi baya na lipi jema, Je kitu ni chema kwa sababu Mungu amesema ni chema?

Kama ndiyo — basi maadili ni arbitrary (yanaweza kubadilika kulingana na amri).

Je Mungu anakisema ni chema kwa sababu tayari ni chema?

Kama ndiyo — basi kuna kiwango cha wema kinachojitegemea, ambacho kipo juu ya Mungu.

Mwisho, Kama Mungu ameumba mfumo mzima wa asili, sheria zake, ubongo wa Binadamu, mazingira yake na mipaka yake, je free will ni halisi au ni ndani ya mipaka iliyowekwa tayari?

Kama Mungu ndiye muamuzi wa mwisho wa lipi baya na lipi jema na msingi ni utiifu badala ya matokeo, basi free will inakuwa ni uchaguzi kati ya utiifu na adhabu, si uhuru kamili wa kimaamuzi.

Hitimisho: Maumivu ni sehemu ya mfumo wa kiasili wa kuendesha uhai, Uovu ni tafsiri ya kibinadamu juu ya maumivu hayo.

Tatizo si kwa nini Uovu upo, bali kwa nini mfumo unaozalisha mateso ungeundwa na Mungu mwenye sifa za upendo na uwezo wote.

Dobzhansky
:
Nothing in biology makes sense except in the light of evolution.”
 
Hakuna shilingi yenye upande Moja
ili kuwe na juu lazima kuwe na chini
ili kuwe na kulia lazima kuwe na kushoto
ili kuwe na mwanga lazima kuwe na giza
ili kuwe na wema lazima kuwe na uovu
 
Uko sahihi kabisa

Nature inatula ili iweze kujinufaisha katika mfumo wake

Yaani Kwa Uhalisia ni kwamba sisi ni chakula Cha Nature ili iweze kujiendesha katika mhimili wake so kuzaliana kwetu Kwa Nature hiyo ni furaha maana inakuwa Ina uhakika wa kujipatia chakula Cha kutosha
 
Hakuna shilingi yenye upande Moja
ili kuwe na juu lazima kuwe na chini
ili kuwe na kulia lazima kuwe na kushoto
ili kuwe na mwanga lazima kuwe na giza
ili kuwe na wema lazima kuwe na uovu
Kwa nini wema utegemee uovu?

Kwani wema hauwezi kutendeka bila uovu?

Kama uovu ni chukizo mbele ya Mungu ingepaswa atunyime uwezo wa kutenda uovu.

Kama ni lazima wema utegemee uovu, basi huyo Mungu hapaswi kuchukizwa na uovu.
 
ili mtu aonekane ni mrefu lazima alinganishwe na wafupi.
Kama watu wote duniani wangekuwa warefu wa kimo sawa basi kusingekuwa na hiyo concept ya mtu mrefu au mfupi,,,ingekuwa watu ni watu tu.

ili kuwe na mwanaume lazima kuwe na mwanamke, ingekuwa watu wote duniani ni wanaume basi hata Hilo neno 'mwanaume' lisingekuwepo maana hiyo concept inalinganisha jinsia.

Kusingekuwa na uovu, hata Hilo neno wema lisingekuwepo na hamna mtu angejua kama jambo flani linalotendeka ni jema au la, kwa maana hatokuwa na idea ya kitu cha tofauti na kinachotendeka.

Ukishajua Kuna uovu basi ndipo utajua pia Kuna wema.
 
Hii ni kweli katika Dunia tunayoishi, yaani kwamba vitu vinaishi in pairs, and they are heterogeneous, lakini kumbuka our world is the only reality of life we know.

Kuna uwezekano kabisa kwamba kukawa na aina nyingine ya maisha ambayo things do not exists in pairs and they are perfectly homogeneous, ishu ni kwamba hatujaweza kugundua.

Kwa mantiki hiyo ni kwamba Uovu Unaweza kuwapo kwa kujitegemea, lakini pia Wema waweza kuwapo kwa kujitegemea, and for me i believe that if science and technology is used to the maximum of its full potentials, a heaven can be created where theres unimaginable perfection of goodness such that evil will never even be remembered to have once existed.
 
Nakubaliana na wewe kwenye point moja muhimu sana:
Ni kweli kabisa kwamba dunia tunayoijua si lazima iwe ndiyo reality pekee inayowezekana.
Lakini hoja yangu haikuwa kuhusu uwezekano wa ulimwengu mwingine — ilikuwa kuhusu logic ya concept yenyewe.
Hata kama kuna aina ya maisha ambayo ni perfectly homogeneous, bado kuna swali la msingi:
👉 Kama hakuna tofauti yoyote, je “utambuzi” wa kitu unatokea vipi?
Kwa sababu concept hutokea pale panapokuwa na distinction.
Bila distinction hakuna definition.
Kwa mfano:
Kama kuna dunia yenye “wema mtupu” bila uwezekano wa uovu —
Je hilo “wema” litaitwaje wema?
Kwa sababu:
Halilinganishwi na kitu kingine
Halichaguliwi juu ya kitu kingine
Halitofautishwi na kitu kingine
Litakuwa tu hali ya kawaida (default state), si maadili.
Hapa ndipo wanafalsafa kama Plato walipojadili kwamba wema unaweza kuwa “form” ya juu kabisa, lakini hata yeye alitumia tofauti kuuelezea.
Na pia Gottfried Wilhelm Leibniz alizungumzia uwezekano wa “best possible world,” lakini bado kulikuwa na mjadala wa kwanini uovu unaonekana kuwepo.
Point yangu ni hii:
Hata kama scientifically tunaweza ku-create environment yenye perfection,
concept ya “perfection” bado inatokana na kulinganisha na imperfection.
Bila possibility ya tofauti, hakuna maana.
Kwa hiyo swali si kama uovu unaweza kuondoka, bali je “wema” utaendelea kuitwa wema kama hakuna hata possibility ya kinyume chake?
Na hapo ndipo mjadala unakuwa wa epistemology (jinsi tunavyojua) si ontology (kitu kuwepo).
Nadhani hapa tunatofautiana si kwenye imagination ya future, bali kwenye logic ya meaning.
Lakini hoja yako ya science ku-create heaven ni interesting sana —
swali litakuwa: je hiyo heaven itakuwa moral goodness au engineered comfort?
Hapo ndipo mjadala unakuwa mzito zaidi 😄
 
Yes, that is a very intellectually interesting and fascinating question.

Kuna Sehemu niliwahi kusoma nikakutana na hili swali: is the universe conscious? Kwa mtazamo wangu, naweza kusema kwamba ulimwengu una consciousness kwa sababu sisi binadamu tuna consciousness, na sisi ni sehemu ya ulimwengu. Consciousness yetu si kitu kilicho nje ya ulimwengu, bali ni expression ya ulimwengu kupitia sisi.

Kwa hiyo, kama “heaven” itakuwa matokeo ya sayansi kuondoa ubaya wote na kuunda mazingira ya wema wa kudumu, basi hilo linaweza kuonekana kama engineered comfort. Lakini pia, kwa mtazamo mwingine, linaweza kuwa moral goodness iliyotokana na uwezo wa viumbe wenye utashi na akili. Kwa maana hiyo, haitakuwa kitu bandia kisicho na maana, bali ni hatua ya ulimwengu kujipanga kuelekea hali yenye kupunguza mateso na kuongeza furaha na amani.

Kwa hiyo, kwangu, engineered comfort na moral goodness haipaswi kuonekana kama vitu vinavyopingana.

Kama engineered comfort inatokana na maamuzi ya kimaadili ya viumbe wenye consciousness kupunguza mateso, basi hiyo yenyewe ni expression ya moral goodness. Hivyo, MBINGU ya namna hiyo haitakuwa tu comfort iliyotengenezwa, bali itakuwa ni ACHIEVEMENT ya kimaadili na kiakili ya ulimwengu kupitia viumbe wake.
 
I agree consciousness yetu ni expression ya ulimwengu kujitambua.
We are a way of the universe knowing itself.
We didn't come into the universe, we've grown out of it. If the universe is a tree, we are not a bird sitting on its branch, we are the branch itself.

Baruch Spinoza alisema Mungu/Asili ni kitu kimoja (substance) ambacho kila kitu ni expression yake.
Kwa hiyo ninakuelewa unaposema:
Kama sisi ni sehemu ya ulimwengu, basi mafanikio yetu ya kimaadili ni mafanikio ya ulimwengu wenyewe.

Lakini hapa kuna swali la muhimu sana
Tukiitengeneza hiyo heaven, na Kama “heaven” hiyo itakuwa hali ambayo:
-Hakuna mateso
-Hakuna uwezekano wa uovu
-Hakuna choice ya kufanya mabaya

Je, bado tutakuwa na maadili?
Kwa sababu maadili yana maana pale ambapo kuna possibility ya kuchagua vinginevyo.
Kama hakuna possibility ya uovu,
basi wema hautakuwa choice — utakuwa necessity.
Na pale ambapo kitu ni necessity, si maadili tena — ni condition tu.
Hoja yangu sio kwamba engineered comfort haiwezi kuwa moral achievement.
Hoja yangu ni hii:
Je moral goodness inaendelea kuwa “moral” kama hakuna tena risk, struggle, au possibility ya kushindwa na kufanya evil?

Kwa mfano:
Kama mtu hawezi kabisa kusema uongo,
je tunamsifu kwa kuwa mkweli?
Au ukweli wake ni default state tu?
Hapa ndipo Kuna distinction:
Engineered comfort inaweza kuondoa mateso.
Lakini moral greatness mara nyingi hutokea katika uwezekano wa kufanya mabaya lakini kuchagua mema.

Bila tension hiyo, je maadili yatabaki na uzito wake?

Kwa hiyo maybe tofauti yetu sio kuhusu heaven kuwezekana au la.
ila ni kuhusu:
Je perfection ya kimaadili inahitaji freedom ya kupotoka?
Au inaweza kuwepo bila possibility ya kinyume chake?
Hapo ndipo mjadala unakuwa wa kina sana — kati ya necessity na freedom.
 
Ndio ndio nakupata sana mkuu.

Kwa mtazamo wangu naiona dunia ilipo sasa ina matatizo mengi ya kisaikolojia ambayo Binadamu huyatengeza wenyewe na mengi ndiyo chanzo cha UBAYA, na kimsingi ni ishu ya matumizi ya resources kwa ajili ya kuishi.

Sasa kwenye ile "perfect heaven" kutakuwa na plenty and abundant resources, na Teknolojia itakuwa imeimarik kwa viwango vya juu yaani mtu yeyote yule atakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwa kutumia rasilimali zisizo na kikomo, hapo hakuta kuwa na wivu, kiburi, matabaka, yaani hakuna kuboeka (full marahaa).

Hakuta kuwa tena na uovu wa asili kama matetemeko ya ardhi, milipuko ya volcano, backteria na virus wataishi ila hawatakuwa na madhara kwenye mwili wa Binadamu na viumbe wengine. Hii ni kutka na maendeleo ya viwango vya juu vya Teknolojia.

Kwa mantiki hiyo ni kwamba, WEMA (FURAHA na AMANI) utakuwa ni default state, na hakutakuwa tena na mazingira ya kutengeneza UOVU.

Neno maadili halitakuwa na mantiki tena, kwasababu UOVU umekwisha ondolewa kabisa.

Uhuru (FREEDOM) utakuwapo lakini hautokuwa juu ya kuchagua kufanya jema au baya, ila kwenye mambo mengine.

EVERY PROBLEM IS SOLVED, EVERYONE IS SEARCHING FOR MORE HAPPINESS AND PEACE WITHOUT THE POSSIBILITY OF HARMING.

HONESTLY HII NI "SCIENCE FICTION" sifahamu kama itaweza kufikiwa.
 
Back
Top Bottom