MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wakati akiongea kwenye kipindi cha Mkasi cha Salama Jabir, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu alisema kipimo kikubwa cha wanasiasa cha kukubalika au kutokubalika katika nchi yetu ni kuangalia upande yaliko makundi ya taasisi za dini na NGOs kubwa.
Tundu Lissu alienda mbali zaidi na kudai hata Mchakato wa Katiba Mpya ulidoda pale tu taasisi za dini na NGOs zilipojitokeza kwenye vyombo vya habari na kuupinga na pia zikasusia kwenye Sherehe ya Makabidhiano ya Katiba iliyopendekewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani zilivyo na nguvu nchini.
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na hoja ya Tundu Lissu.
Fast forward mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu 2015. Tumeanza kuwasikia viongozi wa UKAWA wakilalamika sana na kuwataka Watanzania wajitokeze ili kupinga kile wanachodai kinachofanywa na serikali ya Rais Magufuli ili kuua demokrasia.
Kila mara wakijitokeza kwenye vyombo vya habari utawasikia wakisema, ‘’tunaomba mtuunge mkono, tunaomba mtuunge mkono’’.
Kwa sasa ni miezi zaidi ya sita wakiomba waungwe mkono lakini hakuna Taasisi yoyote kubwa ya dini au NGOs kubwa zimejitokeza kutoa tamko lolote kuhusu kuunga mkono maombi ya viongozi wa UKAWA.
Hakuna statesman/woman aliyejitokeza na kuunga mkono maombi ya viongozi wa UKAWA .
Kutoungwa mkono kwa UKAWA inamaanisha kuwa Taasisi za Dini na NGOs kubwa zinakubaliana na anachokifanya Rais Magufuli.
Mambo gani ambayo Rais Magufuli ameyafanya na anaendelea kuyafanya ambayo yanazifanya Taasisi za Dini na NGOs zikubaliane na kazi anayoifanya?
Mazingira haya pia yananifanya nijiulize kama tatizo ni viongozi wa UKAWA.
Kwa nini viongozi wa UKAWA wanapuuzwa kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha mchakato wa Katiba Inayopendekezwa ambayo ilipelekea mchakato kudoda?
Nini kimetokea kwenye kambi ya UKAWA?
Hata Zitto Kabwe aliyesema yuko tayari kufa kwa kupigania demokrasia kwa sasa yuko kimya na duru za kisiasa zinasema wazee ambao ni statesman wamemshauri apunguze mihemko na jazba za kisiasa kama anataka kufika mbali kisiasa. The man has gone to sleep in order to save his breath!