Hollywood Mentalities.
Ni dhana ambayo imewateka wasomi, wachumi, wanasiasa, wasanii & wakesha hoi barani Afrika na kuwaganda vichwani kama yule mzee aliyempanda mgongoni Sindbad katika ngano za kale na kukataa kushuka.
Humu pia huo ugonjwa umo. Tarehe ya kuzaliwa ya kazi gani?. Logic au mfumo sahihi wa kufikiri ni kufahamu umri--siyo tarehe ya kuzaliwa ya kiumbe chochote hai. Hilo la Tarehe ni suala binafsi, kutafuta ujiko (wishing's) ziso--na mantiki no orodha inaendelea...
Birthday parties Ni tabia inayotokana na utamaduni wa kuiga mifumo ya kitamaduni, sheria, utawala, na demokrasia ya nchi nyingine huku tukidharau uwezo wetu wa kuunda mifumo yetu binafsi ya Maisha.
Ni kuhasiwa kisaikolojia. Zaidi sana ingefana kama sherehe/hafla hizo angefanyiwa Mzazi Mama & Baba kama shukrani kutokana na Malezi bora, upendo na Elimu iso--tokana na u-ingi wa vyeti feki na siyo kumfanyia mtoto mchanga asiye--na upeo ang'avu wowote ule.
I stand to be corrected..