Kwanini tuilaumu serikali kwa matokeo ya kidato cha nne?

Madoki

Senior Member
Sep 2, 2015
101
86
Kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Ibara ya 8. Ibara hii inaipa serikali kuwajibika kwa wananchi na wananchi kujishughulisha katika shughuli za serikali yao.
Sasa jana matokeo ya kidato cha nne yametangazwa na kila mtu ameyaona na kuyafuatilia kadri anavyohusika. tumeona shule zilizofanya vizuri na zilizofanya vibaya kwa mujibu wao walivyozijaji. Waswahili wanasema kila mtu ana kwao, sasa ile sekondari ya kijijini kwenu umeifuatilia na kujua matokeo yake? Je changamoto zake umeziona? Umezisemea popote pale? hata hapa jf ambapo tunaona viongozi na vigogo wa nchi hii wanatembelea sana na mara kwa mara kujua kinachoendelea humu ndani?
Kabla hatujaanza kuilaumu serikali wewe umetimiza wajibu wako kujishughulisha na shughuli za serikali katika swala la elimu? Uko mjini hapa una uwezo hata wa kujenga chumba kimoja pale kwenu na kukiweka safi, mwalimu wa Hesabu aje kupanga hapo na kuwafundisha ndugu zako uliowaacha kule kijijini. Au unafurahia kuona ndugu zako wanapata ziro kwa kuwa walimu hawakai kwa sababu ya mazingira mabovu.
Wito wangu tusiilaumu serikali, tuanze na sisi kwa kuzisemea shule za vijijini kwetu humu JF changamoto zake na matatizo yake na kama tunauwezo wa kuzitatua kadri Mungu alivyokuwezesha kwa kujenga nyumba ya Mwalimu, kununua chaki, au kalibrary na kuweka vitabu vichache wadogo zetu wakavitumia private hata kwa kuchangia mia tano kwa mwezi, hapo utakua umefanya jambo la kheri. Tukumbuke nyumbani ni nyumbani hata kama ni kijijijini. Ni hayo tu, tusiongozwe na Mizuka au matukio ndo tunakurupuka kutoa maamuzi.
 
Back
Top Bottom