Kwanini tuendelee kuwa na bunge? Ikulu haiogopi bunge!

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Kila baada ya miaka mitano wananchi wanafurika kwenye vituo vya kura kuchagua wabunge na raisi. Wakijua kwamba wabunge hawa watasaidia kuishauri , kuisimamia na kutoa maelekezo yanayotakiwa kutimizwa na serikali.

Serikali chini ya raisi inaunda vyombo mabli mbali kuisaidia kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama vile CAG, Takukuru, TRA, Tanesco, polisi, nk ili kuleta ufanisi.

Leo Takukuru na CAG vyombo vya serikali vimeliambia bunge, Mhongo, Tibaijuka, Maswi, Werema, Chenge, Ngeleja, ni wezi au wahujumu wa mali ya umma wanatakiwa kupewa adhabu pamoja na kufukuzwa kazi zao. Hii ni baada ya wabunge kuipitia ripoti ya PAC, TRA, PCCB, na CAG na kurithika pasipo shaka kuwa hawa hawafai tena kulitumikia taifa kwa kodi za waTZ.

Leo inashangaza sana kusikia ikulu eti inafanya uchunguzi kabla haijawafukuza. Je kuna umuhimu gani wa kuwa na bunge na serikali hailiamini bunge?

Je itakuwaje wezi watakaporudi dodoma bunge la january/february na kuendelea na kazi zao? Je itakuwaje wizi mwingine kutokea kama huu wa bomba la mafuta unaokuja? Je kwanini tuwe na bunge kama hakuna kuheshimiana na kuaminiana.

Je kama ikulu inakataa kuwajibisha wezi wananchi wafanye nini?
Wakae wanashangaa tu
wawapige kelele mpaka wezi watoke
walalamike tu na kusahau
waaznishe maandamano mpaka ikulu kushinikiza wezi wafukuzwe
au wamwachie Mungu kwani unyonge wetu ndio bakara yetu?

Mimi nasema hapana, ikulu ikishindwa kuchukua hatua ndani ya mwezi mmoja wananchi wanahaki kufanya lolote kushikiniza hawa wezi watolewe.

Naomba sana Raisi Jakaya Kikwete atumia busara asisubiri mpaka ifike siku analazimishwa kutoa maamuzi.

Chief Mkwawa- kifo cha chief kwa ajili ya kutetea watu-usipime uji wa moto kwa vidole.
 
Mkuu hapa tulipo hakuna msafi sasa wanaambiana you scratch my back I will scrath yours.
 
kama ikulu yenyewe imetajwa; maswali ya nini? Kitakacho tokea na kutokuwa na imani na mkuu wa kaya. Itatubidi tumuondoe kwanza yeye!
 
Back
Top Bottom