mafimboo
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 2,415
- 977
maskini nchi yangu kwanini huendelei licha ya kuzungukwa na malighafi za kila namna ,mbuga za wanyama,gesi,madini na n.k,ghafla nikakumbuka hadithi ya watoto mapacha waliorithishwa mali na baba yao,Doto alirithishwa shamba na kurwa alirithishwa jembe ,badala ya kushirikiana walime ,kila mmoja akaanza kujiona bora kuliko mwezie,doto hakutaka kutumia jembe la kurwa hata kumruhusu kurwa alime shambani mwake na kurwa hakupenda kulilima shamba la kurwa hata kumuazima jembe doto alimie ,chuki baina yao ilizidi kuwa kubwa licha ya kupewa usiwa na baba yao wa kupendana,mwishoni shamba liliota mbigiri na vichaka na jembe likapata kutu na kuharibika,hadithi hii ikanikumbusha utawala wa awamu ya tano wa tz & wapinzani,wahenga walisema nyota njema huonekana asubuhi,kipaumbele cha kwanza cha serikali ikawa kupambana na wapinzani na silaha ya kwanza ni kuzima matangazo ya bunge ili wasionekane wakiiumbua serikali,wapinzani wakagoma wakanzisha vurugu,silaha ya pili ikawa ni kuwaminya bungeni wasitoe hoja zenye mashiko wapinzani wakamua kutoka nje ya bunge,silaha ya mwisho na mbaya zaidi ni kuwafunga midomo na kuwapeleka mbele ya pilato kwa kila neno watakalo lionge likiwa haliwafurahishi watawala ,miaka yote itakuwa ni kupambana na wapinzani badala ya kuhangaika na maendeleo ya nchi na rasilimali tulizonazo,hivi watawala hawajifunzi kutoka nchi za ulimwengu wa kwanza ,unaingia madarakani na kuanzisha vita na wapinzani ndilo wananchi tulilokutuma,wananchi hatukuwatuma kuzima matangazo ya bunge tumewatuma maendeleo,KWA DALILI HIZI NCHI HAIWEZI KUENDELENDELEA HATA KWA MACHOZI, Duniani koteserikali inayojikita kwenye kupambana na wapinzani na kuwa kaidi na kali HAIWEZI KULETA MAENDELEO